
FURSA YA INTERNSHIP – SALES & MARKETING
GLOBAL TV ONLINE inawakaribisha vijana wenye ndoto za kujenga taaluma katika eneo la Sales & Marketing kujiunga na programu ya Internship ndani ya Idara ya Masoko.
Ikiwa una shauku ya kujifunza, kukuza uwezo wako wa mauzo na masoko, pamoja na kupata uzoefu katika kampuni kubwa ya habari na maudhui ya kidijitali, hii ni nafasi yako!
SIFA ZA MWOMBAJI:
✅ Awe amehitimu Chuo cha Kati au Chuo Kikuu katika masomo ya Sales & Marketing au fani zinazohusiana.
✅ Awe nadhifu, mwenye maadili mema na nidhamu ya kazi.
✅ Awe na uwezo mzuri wa kuwasiliana kwa Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha.
✅ Awe anaishi katika mojawapo ya miji hii:
📍 Dar es Salaam
📍 Arusha
📍 Dodoma
📍 Mwanza
✅ Awe tayari kufanya Internship kwa lengo la kujifunza na kupata uzoefu wa kazi.
UTAKACHOPATA:
🔹 Mafunzo ya vitendo kutoka kwa wataalamu wa masoko.
🔹 Uzoefu wa kufanya kazi katika kampuni ya media yenye mamilioni ya wasomaji na watazamaji.
🔹 Msaada wa gharama za usafiri kipindi cha mafunzo.
🔹 Fursa ya kupata Commission kulingana na matokeo ya kazi.
🌟 Je, unaamini una sifa hizi?
Usisubiri kesho — chukua hatua leo na anza safari yako ya taaluma pamoja na Global TV Online!
📧 Tuma Barua ya Maombi pamoja na CV yako kupitia:
[email protected]
📞 Kwa maelezo zaidi:
0799 444 036
GLOBAL TV ONLINE
“Kimbilio la Wasio na Sauti”