×

Yanga Yashuka Bukombe Kwa Kishindo, Dkt. Biteko Apewa Heshima Maalum – Picha

Rais wa Klabu yetu Eng. Hersi Said, akimkabidhi jezi mwenyeji wetu, Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Naibu Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Dkt. Doto Biteko.

Klabu ya Yanga imeandika historia mpya baada ya kupeleka tamasha lake la Wiki ya Mwananchi 2026 nje ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa hafla hiyo.

Yanga leo Agosti 4, 2026 ipo Ushirombo, Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, kwa ajili ya uzinduzi na maadhimisho ya Wiki ya Mwananchi, tukio linalolenga kuwakutanisha mashabiki, wanachama na viongozi wa klabu hiyo katika maeneo mbalimbali nchini.

Katika tukio hilo, Rais wa Klabu ya Yanga SC, Eng. Hersi Said, alimkabidhi jezi ya klabu hiyo Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Naibu Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt. Doto Biteko, katika hafla iliyofanyika kwenye Uwanja wa Bukombe.

Hatua ya kupeleka Wiki ya Mwananchi mkoani Geita imeelezwa kuwa ni sehemu ya juhudi za Yanga za kuwasogeza karibu mashabiki wake waliopo mikoa mbalimbali nchini na kuendelea kujenga umoja kati ya klabu na wanachama wake.

Tamasha la mwaka huu limekuwa la kipekee kutokana na kufanyika nje ya Dar es Salaam, likiwa ishara ya upanuzi wa ushiriki wa mashabiki wa Yanga kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania.

 

Leave a Comment