×

Picha za Zuchu Akiwa Mjamzito Zatikisa Mitandao, Diamond Avunja Ukimya – (Picha +Video)

Msanii wa Bongo Fleva, Nassib Abdul maarufu Diamond Platnumz ameibua mjadala mkubwa mitandaoni baada ya kushiriki picha inayomuonesha mpenzi wake, Zuhura Othman maarufu Zuchu, akiwa na ujauzito, jambo lililowafanya mashabiki wengi kuamini kuwa wawili hao wanatarajia kupata mtoto.

Diamond alichapisha picha hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram akiambatanisha na ujumbe unaosema, “New Heart Beats in the Family,” kauli ambayo wengi wameitafsiri kuwa ni ishara ya ujio wa mwanafamilia mpya.

Naye Zuchu alichapisha picha hizo leo Julai 30, 2026 kwenye ukurasa wake wa Instagram, akiandika, “Growing Love and Eating for Two, pls be a chubby baby,” ujumbe ulioongeza uzito wa tafsiri kuwa huenda msanii huyo anatarajia kujifungua mtoto.

Hadi sasa, Diamond na Zuchu hawajatoa maelezo ya ziada kuthibitisha moja kwa moja iwapo kweli wanatarajia mtoto, lakini machapisho yao yameendelea kuzua gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii.

Mashabiki, wasanii na wadau mbalimbali wamefurika kwenye kurasa zao za kijamii wakitoa pongezi na salamu za heri, huku wengine wakisubiri wawili hao kutoa tamko rasmi kuhusu taarifa hizo.

Iwapo taarifa hizo zitathibitishwa, atakuwa ni mtoto wa kwanza wa Diamond na Zuchu kama wanandoa, jambo ambalo litakuwa hatua nyingine muhimu katika maisha yao ya kimapenzi ambayo yamekuwa yakifuatiliwa kwa karibu na mashabiki ndani na nje ya Tanzania.

Leave a Comment