
Halmashauri ya Wilaya ya Mafia imetangaza nafasi mbili (2) za ajira kwa kada ya Nahodha Daraja la II (Skipper) na kuwakaribisha Watanzania wenye sifa na uwezo kuwasilisha maombi yao.
Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa Julai 30, 2026, waombaji wanatakiwa kuwa wamehitimu Kidato cha IV au VI na kuwa na Stashahada (Diploma NTA Level 6) ya Unahodha na Uvuvi (Master Fisherman) kutoka Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
Majukumu ya kazi
Miongoni mwa majukumu ya mwombaji atakayefaulu ni:
- Kuendesha boti za doria.
- Kuongoza na kuendesha boti au meli ndogo.
- Kushiriki doria za baharini na nchi kavu pamoja na doria za Ukanda wa Kiuchumi wa Bahari (EEZ).
- Kusoma na kuwasilisha taarifa za mfumo wa ufuatiliaji wa vyombo vya uvuvi (VMS).
- Kukamata wanaokiuka Sheria na Kanuni za Uvuvi.
- Kutunza kumbukumbu za matumizi ya mafuta ya vyombo vya doria.
- Kushiriki kupanga matengenezo ya vyombo vya doria na kutekeleza majukumu mengine ya kitaaluma atakayopangiwa.
Masharti muhimu
- Mwombaji awe raia wa Tanzania.
- Asiwe na umri unaozidi miaka 45.
- Mshahara wa nafasi hiyo ni TGS C.
- Waombaji wanapaswa kuambatisha vyeti vyote vinavyohitajika, ikiwemo cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria au Wakili.
- Matokeo ya muda (Provisional Results), Statement of Results na Result Slips hayatakubaliwa.
Maombi yote yanapaswa kutumwa kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) na pia kuambatisha barua ya maombi iliyoelekezwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia.
Mwisho wa kutuma maombi ni Agosti 12, 2026.
Waombaji wamekumbushwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na kuepuka vitendo vya rushwa, kwani mchakato wa ajira unazingatia misingi ya haki, usawa na uwazi.
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MAFIA 30-07-2026