×

Diddy Aongezewa Muda wa Kukaa Gerezani Baada ya Kuzua Ugomvi

Msanii na mfanyabiashara maarufu wa muziki Sean ‘Diddy’ Combs ataendelea kutumikia kifungo chake kwa muda mrefu zaidi baada ya mamlaka za magereza nchini Marekani kusogeza mbele tarehe yake ya kuachiliwa huru.

Kwa mujibu wa taarifa za Federal Bureau of Prisons, Diddy sasa anatarajiwa kuachiwa huru Februari 20, 2028, badala ya Januari 2028 kama ilivyokuwa imepangwa hivi karibuni.

Mabadiliko hayo yanakuja baada ya Diddy kuhusishwa na ugomvi uliotokea akiwa gerezani. Ingawa aliwahi kuwekwa kwenye kifungo cha upweke kufuatia tukio hilo, mamlaka hazijatoa maelezo rasmi kuhusu sababu ya kurejesha tena tarehe yake ya kuachiliwa hadi Februari.

Kwa kipindi cha miezi ya karibuni, tarehe ya kuachiliwa kwa Diddy imekuwa ikibadilishwa mara kadhaa. Awali ilikuwa imepangwa katikati ya mwaka, baadaye ikahamishwa Aprili, kisha Februari, ikasogezwa Januari, na sasa imerejeshwa tena Februari 2028.

Diddy anatumikia kifungo cha miezi 50 jela baada ya kutiwa hatiani mwezi Oktoba 2025 kwa makosa mawili yanayohusiana na usafirishaji wa watu kwa madhumuni ya ukahaba.

Leave a Comment