×

Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Yatangaza Nafasi 2 za Kazi

Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imetangaza nafasi mbili za kazi kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi ya Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II (Office Management Secretary Grade II).

Tangazo hilo lililotolewa tarehe 4 Agosti 2026 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga linaeleza kuwa waombaji wanaotakiwa ni wahitimu wa Kidato cha Nne au Kidato cha Sita wenye Stashahada ya Uhazili (Secretarial Studies) NTA Level 6.

Majukumu ya kazi

Miongoni mwa majukumu ya nafasi hiyo ni:

  • Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida pamoja na za siri;
  • Kupokea wageni na kuwaelekeza wanapoweza kusaidiwa;
  • Kutunza kumbukumbu za matukio, miadi, vikao na ratiba za kazi;
  • Kutafuta na kusambaza majalada na nyaraka zinazohitajika;
  • Kuandaa maandalizi ya vikao mbalimbali;
  • Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi;
  • Kufanya majukumu mengine atakayopangiwa na mkuu wa kazi.

Sifa za mwombaji

Mwombaji anatakiwa:

  • Awe raia wa Tanzania;
  • Awe na umri usiozidi miaka 45;
  • Awe na Stashahada ya Uhazili (NTA Level 6);
  • Awe amefaulu Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza kwa kasi ya maneno 80 kwa dakika;
  • Awe na ujuzi wa matumizi ya programu za kompyuta za ofisi kama Word, Excel, PowerPoint, Internet, E-mail na Publisher.

Nafasi hiyo ina kiwango cha mshahara cha TGS C.

Waombaji wanatakiwa kuambatanisha vyeti vya elimu vilivyothibitishwa pamoja na barua ya maombi ya kazi iliyosainiwa.

Maombi yote yawasilishwe kupitia mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia:
https://portal.ajira.go.tz/

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 18 Agosti 2026.

Barua ya maombi ielekezwe kwa:

Mkurugenzi wa Manispaa
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga
S.L.P 187, Rukwa

Leave a Comment