×

Viongozi Wa Chadema, TLS Na ACT Wafika Mahakamani Kufuatilia Kesi Ya Lissu – Video

DAR ES SALAAM: Viongozi na baadhi ya wadau wa siasa na sheria leo Agosti 10, 2026 wamefika katika Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, kufuatilia mwenendo wa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu.

Viongozi waandamizi wa CHADEMA, wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara, John Heche, wameonekana ndani ya chumba cha Mahakama Kuu wakifuatilia mwenendo wa shauri hilo.

Miongoni mwa waliofika mahakamani hapo ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, ambaye amefika kufuatilia kesi hiyo inayovuta hisia za umma.

Aidha, Mchungaji Peter Msigwa, ambaye ni kada wa CHADEMA, naye ni miongoni mwa waliohudhuria mahakamani hapo.

Kwa upande mwingine, kada wa ACT Wazalendo, Luhaga Joelson Mpina, pia amefika Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam kufuatilia kesi hiyo.

Kesi ya Lissu inaendelea kusikilizwa mbele ya Jopo la Majaji watatu wa Mahakama Kuu, huku mwenendo wake ukiendelea kufuatiliwa kwa karibu na viongozi wa kisiasa, wanasheria na wananchi.

Mwenendo wa kesi hiyo unaendelea mahakamani.

 

Leave a Comment