
Kesi inayomkabili Tundu Lissu imeahirishwa hadi kesho, Alhamisi Agosti 13, 2026 baada ya upande wa Jamhuri kuomba muda zaidi kwa madai kuwa haujajiandaa na shahidi mwingine.
Akizungumza mahakamani, Lissu ameomba Mahakama izingatie amri yake ya awali iliyowataka upande wa Jamhuri kuwasilisha mashahidi wawili.
“Tumechelewa sana, na sio kwa sababu zangu, ni kwa sababu zao. Mimi naendelea kukaa gerezani na sina hatia. Kuanzia kesho waje na mashahidi wa kutosha,” amesema Lissu.
Baada ya kusikiliza maombi hayo, Jaji ameahirisha shauri hilo hadi kesho saa 3:00 asubuhi, ambapo mwenendo wa kesi hiyo utaendelea.