×

Spider-Man Yaendelea Kuvunja Rekodi Katika Doko la Dunia

Filamu mpya ya Spider-Man, Spider-Man: Brand New Day, imeendelea kufanya vizuri katika soko la kimataifa baada ya kuweka rekodi mpya nchini India.

Filamu hiyo inayomshirikisha Tom Holland katika nafasi ya Spider-Man imekuwa filamu ya Hollywood iliyofanya vizuri zaidi katika historia ya soko la India, baada ya kuipita Avatar: The Way of Water ya mwongozaji James Cameron.

Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni, Spider-Man: Brand New Day imekusanya zaidi ya rupee milioni 5,000 nchini India ndani ya siku 12 tangu kuanza kuonyeshwa.

Licha ya mapato kupungua katika baadhi ya siku za wiki, filamu hiyo imeendelea kuvuta idadi kubwa ya watazamaji katika kumbi za sinema, hali inayoendelea kuifanya kuwa miongoni mwa filamu za Hollywood zilizofanya vizuri zaidi nchini humo mwaka huu.

Umaarufu wa mhusika Spider-Man pamoja na jina la Tom Holland umetajwa kuwa miongoni mwa sababu zinazochangia filamu hiyo kuendelea kuvutia mashabiki katika masoko mbalimbali duniani.

Mbali na mafanikio nchini India, filamu hiyo pia imeendelea kufanya vizuri katika soko la kimataifa, ikiwa tayari imevuka dola bilioni moja katika mapato kutoka masoko ya nje ya Marekani na Canada ndani ya siku 12.

Kiwango hicho ni sawa na zaidi ya TSh trilioni 2.6, kwa makadirio ya dola moja ya Marekani kuwa karibu TSh 2,600.

Mafanikio ya Spider-Man: Brand New Day yanaendelea kuonyesha ukubwa wa soko la filamu nje ya Marekani, huku watazamaji wa kimataifa wakizidi kuwa sehemu muhimu katika kuongeza mapato ya filamu za Hollywood.

Leave a Comment