
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na CEO wa Konde Music Worldwide, Harmonize, ameibua hisia miongoni mwa mashabiki baada ya kuonyesha mjengo wake mpya alioujenga eneo la Salasala, nje ya jiji la Dar es Salaam.
Harmonize amefanya hivyo usiku wa kuamkia leo, Agosti 17, 2026, kupitia mitandao ya kijamii, ambapo alishirikisha picha za nyumba hiyo huku akieleza kuwa ni sehemu ya kusherehekea mafanikio yake mapya.
Katika ujumbe wake, Harmonize aliandika: “Tunaposherehekea muziki mpya wa #Beautiful 💛 na albamu inayokuja Septemba 4 💛, tunasherehekea pia mjengo mpya 🏠💛.”

Ujumbe huo umefika wakati ambao msanii huyo akijiandaa kuachia muziki mpya pamoja na album yake inayotarajiwa kutoka Septemba 4, 2026.
Baada ya Harmonize kuonyesha mjengo huo, mashabiki wake mbalimbali walijitokeza kwenye mitandao ya kijamii kumpongeza kwa hatua hiyo, huku wengi wakimtakia mafanikio zaidi katika kazi yake na maisha kwa ujumla.
Mjengo huo umeongeza gumzo miongoni mwa mashabiki, ambao wameendelea kufuatilia kwa karibu maisha na mafanikio ya msanii huyo.