×

Video: Shigongo Aishukuru Serikali kwa Ujenzi wa Shule Mpya Mizororo

BUCHOSA: Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo, ameishukuru Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi Mizororo, iliyopo Kata ya Kalebezo katika Jimbo la Buchosa.

Shigongo ametoa shukrani hizo baada ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Mwang’onda, kukagua mradi huo na kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo.

Amesema ujenzi wa shule hiyo ni sehemu ya jitihada za Serikali katika kuboresha mazingira ya elimu na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii.

Kwa upande wake, Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2026 zimeridhishwa na usimamizi pamoja na utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Jimbo la Buchosa, ikiwemo mradi huo wa ujenzi wa Shule ya Msingi Mizororo.

Ujenzi wa shule hiyo unatarajiwa kuongeza fursa kwa watoto wa eneo hilo kupata elimu katika mazingira bora na kupunguza changamoto ya upatikanaji wa miundombinu ya elimu katika Kata ya Kalebezo.

Leave a Comment