
Klabu ya Simba SC inayonolewa na Kocha , Steve Barker ina kibarua kizito kukabiliana na Pamba Jiji FC kwenye NBC Premier League, Agosti 19,2026 ikiwakosa nyota wake muhimu wawili.
Mchezo huu utakuwa ni wa pili kwa timu zote mbili unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa CCM Kirumba saa 10:15 jioni.
Mnyama anatarajiwa kukosa huduma ya mlinda mlango namba moja Mamadou Kasali huku Hussen Abel kipa namba mbili akitarajiwa kupewa mikoba yake katika dakika 90 za kusaka ushindi.
Sababu kubwa ya Kassali kukosekana ni kupata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar Mbali na Kasali, beki David Kameta Duchu hatakuwa sehemu ya kikosi.
Beki huyu mbavu ya kulia alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 53 mchezo dhidi ya Kagera Sugar kwa kosa la kumchezea faulo beki David Luhende ambapo FVS (Footbal Video Support) ilitumika kwa mwamuzi wa kati Saad Mrope kufanya maamuzi.
Lunyamadzo Mlyuka