×

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: Fenerbahce, Lyon Kwenye Vita ya Kufuzu

Leo usiku, Jumanne Agosti 18, 2026, uwanja wa Şükrü Saraçoğlu utakuwa jukwaa la mojawapo ya mechi kubwa ya msimu wa kufuzu kwa UEFA Champions League. Fenerbahce, mabingwa wa zamani wa Uturuki, watapokea ugeni wa Lyon kutoka Ufaransa katika mchezo wa kwanza ya duru ya mwisho ya kufuzu.

Fenerbahce wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na kiu kubwa ya mafanikio. Kocha wao Domenico Tedesco alichukua nafasi baada ya kuondoka kwa Jose Mourinho mwaka jana, na sasa anataka kuithibitisha ubora wa timu hii mbele ya mashabiki wake wa nyumbani.

Safari yao ya kufuzu imekuwa nzuri hadi sasa, wakipita Gornik Zabrze na Sturm Graz, ingawa kiwango chao cha hivi karibuni kimetikiswa kidogo na kushindwa dhidi ya Genclerbirligi. Habari njema kwao ni kurejea kwa kipa nambari moja Ederson, ingawa bado watakosa Mert Gunok na Jayden Oosterwolde.

Upande wa pili, Lyon wanafika Istanbul wakiwa na kasi kubwa baada ya msimu mgumu wa kifedha uliowahi kuwatishia hata kushushwa daraja. Chini ya uongozi mpya, timu imeonyesha nguvu tena, ikimalizia nafasi ya nne katika Ligue 1 na kuja na ushindi mkubwa wa 3-0 dhidi ya Sparta Prague katika raundi iliyopita.

Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema.  Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Hata hivyo, majeraha ya wachezaji watatu muhimu Pavel Sulc, Nicolas Tagliafico na Mads Bidstrup yanaweza kuathiri mpangilio wao wa mchezo katika safari hii ngumu ya ugenini.

Historia baina ya timu hizi mbili inaonyesha Lyon wakiwa na ubora dhahiri, wakiwa wameshinda mechi nne kati ya tano za mwisho walizocheza dhidi ya Fenerbahce, huku ushindi mmoja tu wa Waturuki ukikosekana katika kumbukumbu za hivi karibuni.

Aidha, takwimu za magoli zinaonyesha mechi zao mara nyingi huwa na mabao mengi, jambo linalowapa mashabiki matarajio ya mchezo wa kusisimua wenye mashambulizi pande zote mbili.

Ukichanganya mambo yote historia ya Lyon, ubora wao wa kimtindo, lakini pia hamasa na faida ya uwanjani kwa Fenerbahce. Matokeo ya leo yatakuwa msingi muhimu kabla ya mchezo wa marudiano utakaofanyika Ufaransa wiki ijayo.

Leave a Comment