×

Video: Mbunge Shigongo Apongeza Serikali kwa Kuboresha Shule ya Kasaji

BUCHOSA: Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo, ameipongeza Serikali kwa hatua ya ujenzi wa miundombinu katika Shule ya Msingi Kasaji, iliyopo Kata ya Kazunzu, Jimbo la Buchosa.

Shigongo amesema miundombinu hiyo inayojengwa katika shule hiyo inaleta matumaini mapya kwa wanafunzi, walimu na wananchi kwa ujumla, huku akiwataka wananchi kuhakikisha wanaitunza na kuilinda ili iweze kutumika kwa muda mrefu.

Amesema uwekezaji katika miundombinu ya elimu ni hatua muhimu katika kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia, hivyo wananchi wanapaswa kuwa sehemu ya kulinda na kusimamia miradi inayotekelezwa katika maeneo yao.

Mbunge huyo pia amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wananchi katika kutekeleza miradi ya maendeleo, akisisitiza kuwa ushirikiano huo ni muhimu katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na maendeleo endelevu.

Leave a Comment