
Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga SC, leo Alhamisi, Agosti 20, 2026, watashuka dimbani kuikabili Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/27.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa katika Uwanja wa KMC Complex, Mwenge jijini Dar es Salaam kuanzia saa 12:30 jioni.
Yanga inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na lengo la kuendeleza mwanzo mzuri wa msimu na kuongeza alama katika msimamo wa ligi, timu hiyo ilianza kampeni zake za ligi kwa ushindi wa 3-1 dhidi ya Namungo FC.

Coastal Union itakuwa na kazi ya kuzuia kasi ya Yanga na kutafuta matokeo mazuri katika mchezo huo wa raundi ya pili.
Mchezo wa leo unatarajiwa kuwa mwingine wa ushindani huku Coastal Union ikitaka kuwa na ushindi baada ya kupoteza mechi ya kwanza ya ligi.
Macho ya mashabiki wa soka nchini yataelekezwa katika uwanja wa KMC Complex kusubiri kuona kama Yanga itaendelea na kasi yake na kuondoka na ushindi mbele ya Coastal Union.
Stori na Haika Urio | GPL – TUDACO