×

Linah Aahidi Burudani ya Kipekee Kwenye Miaka 30 ya Bongo Fleva – Video

DODOMA: Nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Linah Sanga, amefunguka kuhusu maandalizi yake kuelekea shoo ya kusherehekea Miaka 30 ya Bongo Fleva, inayofanyika jijini Dodoma.

Linah amesema mashabiki wanaweza kutarajia burudani ya aina yake, huku akiahidi kuwa amejipanga vyema kwa ajili ya kupanda jukwaani na kutoa burudani pamoja na “sapraiz” mbalimbali.

Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika Chinangali Park, Dodoma, Agosti 22, 2026, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 30 ya muziki wa Bongo Fleva.

Akizungumza kupitia Global TV, Linah pia amefunguka kuhusu historia ya mahusiano yake na msanii Amini, akieleza kuwa tofauti zilizojitokeza baina yao zilikuwa miongoni mwa sababu zilizopelekea kuvunjika kwa uhusiano wao.

Mbali na suala hilo, Linah amezungumzia pia wimbo “Yalaiti”, ambao alishirikishwa na msanii na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mwana FA.

Kwa sasa, Linah ni miongoni mwa wasanii wanaotarajiwa kutoa burudani katika maadhimisho hayo, huku mashabiki wakisubiri kuona “sapraiz” alizoahidi kwa ajili ya shoo hiyo.

Leave a Comment