×

Tanzania Yaendelea Kung’ara Miss World, Latricia Ian Afuzu Top 60

Mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Miss World 2026, Latricia Ian, amefanikiwa kuingia kwenye orodha ya warembo 60 bora katika kipengele cha Top Model, hatua inayomuweka katika nafasi nzuri ya kuwania ushindi wa kipengele hicho nchini Vietnam.

Ian amefuzu miongoni mwa washiriki kutoka mataifa mbalimbali duniani, akiendelea kuiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo yanayowakutanisha warembo kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, fainali ya kipengele cha Top Model inatarajiwa kufanyika Agosti 28, 2026, ambapo warembo hao 60 watashindana katika hatua ya mwisho ya kipengele hicho.

Mbali na Top Model, washiriki wote 111 wanaowakilisha mataifa yao watapata nafasi ya kutembea kwenye jukwaa katika kuwania World Designer Award, huku wakionyesha mitindo na utambulisho wa maeneo yao ya kijiografia.

Kwa upande wa Tanzania, kufuzu kwa Latricia Ian katika Top 60 ni hatua nyingine muhimu katika safari yake ya Miss World 2026, huku akitarajiwa kuendelea kupambana katika hatua zinazofuata za mashindano hayo.

Macho ya mashabiki wa Tanzania sasa yanaelekezwa Agosti 28, wakati Ian atakapokuwa akiwakilisha Tanzania katika hatua ya fainali ya Top Model.

Stori na Ilankize Godfrey | GPL – TUDACO

Leave a Comment