Dar es Salaam, Agosti 24, 2026 – Kampuni ya Coca-Cola Tanzania imezindua rasmi ladha mpya ya kinywaji cha FANTA® Berry nchini Tanzania, ikiwa ni nyongeza katika familia ya vinywaji vya FANTA®.
FANTA® Berry imeelezwa kuwa na ladha ya matunda yenye mvuto, ikilenga kuwapa watumiaji uzoefu mpya wa kinywaji huku ikiendana na utamaduni na nguvu ya vijana nchini Tanzania.
Akizungumza kuhusu uzinduzi huo, Kabula Nshimo, Senior Marketing Manager wa Coca-Cola Tanzania, amesema FANTA® Berry inalenga kuongeza chaguo kwa watumiaji na kukidhi mabadiliko ya mapendeleo yao.
Uzinduzi huo umeambatana na kampeni maalum inayojulikana kama “Kipapli”, ambayo inalenga kuwafikia vijana kupitia muziki, dansi, mitindo, watayarishaji wa maudhui na matukio mbalimbali ya burudani.
Kampeni hiyo pia imehusisha muziki wa Singeli, ambao umeendelea kupata umaarufu mkubwa miongoni mwa vijana nchini Tanzania.

Katika kuufikisha ujumbe huo kwa watumiaji, Coca-Cola Kwanza imeandaa msafara wa matangazo ulioanzia katika kiwanda cha Mikocheni na kupita maeneo mbalimbali ikiwemo Ubungo, Mabibo, Buguruni na Temeke kabla ya kuhitimishwa Mbagala.
Katika maeneo hayo, watumiaji wamepata fursa ya kuonja FANTA® Berry, kushiriki michezo na burudani pamoja na shughuli mbalimbali za kuhamasisha bidhaa hiyo.
Aidha, kampeni hiyo inatarajiwa kuhusisha watayarishaji wa maudhui mitandaoni, changamoto za ubunifu, ushirikiano na influencers pamoja na kampeni ya #KipapliChallenge kwenye mitandao ya kijamii.
Kwa upande wake, David Chait, General Manager wa Coca-Cola Kwanza Ltd, amesema kampuni hiyo inaendelea kuongeza bidhaa zinazokidhi mapendeleo mbalimbali ya Watanzania.
FANTA® Berry sasa inapatikana katika baadhi ya maduka, supermarket, vyuo vikuu, vibanda na maeneo mengine ya biashara nchini Tanzania.
Ladha hiyo mpya inakuja huku FANTA® ikiendelea kuwa na ladha zake maarufu, ikiwemo FANTA® Orange, katika soko la Tanzania.
