×

Quevin Castro Afariki Dunia Baada Ya Kuanguka Uwanjani

Kiungo wa zamani wa West Bromwich Albion, Quévin Castro, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 25 baada ya kuanguka ghafla wakati akiichezea Real Sport Clube katika mchezo wa kirafiki nchini Ureno.

Tukio hilo lilitokea Jumamosi, Agosti 22, 2026, katika mchezo kati ya Real Sport Clube na Estrela da Amadora. Castro alianguka takribani dakika 10 baada ya mchezo kuanza na kupoteza fahamu.

Madaktari waliokuwa uwanjani walitoa huduma ya dharura na kutumia mashine ya kushtua moyo (defibrillator) kabla Castro hajapelekwa hospitalini kwa ajili ya matibabu zaidi.

Hata hivyo, juhudi za kumuokoa hazikufanikiwa na Castro alifariki muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini. Kifo chake kimetikisa soka la Ureno na Uingereza.

Castro alikuwa ameanza maisha yake ya soka nchini Uingereza na baadaye akajiunga na West Bromwich Albion mwaka 2021, ambako alicheza mechi mbili za kikosi cha kwanza. Pia aliwahi kuzichezea klabu kadhaa ikiwemo Burton Albion, Notts County, Gateshead na York City kabla ya kurejea Ureno.

Kifo hicho kimepokelewa kwa huzuni kubwa na klabu alizowahi kuzichezea, huku West Bromwich Albion ikieleza kusikitishwa na kifo cha ghafla cha mchezaji huyo mwenye umri mdogo.

Mchezo ambao Castro alianguka ulisitishwa kufuatia tukio hilo, huku jumuiya ya soka ikiendelea kutoa salamu za pole kwa familia, ndugu, marafiki na klabu yake.

Stori na Haika Urio | GPL – TUDACO

Leave a Comment