×

Ikulu Yathibitisha Dkt. Nchimbi Kujiuzulu Umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepokea na kuridhia ombi la kujiuzulu kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, kuanzia tarehe 4 Septemba 2026.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi leo, Agosti 25, 2026, Rais Samia amekubali ombi hilo la Nchimbi la kujiuzulu nafasi hiyo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa taratibu za kikatiba za kumpata Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwingine zitachukuliwa.

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses M. Kusiluka, tarehe 25 Agosti 2026.

Leave a Comment