×

Video: CCM Yamvua Uanachama Nchimbi Siku Moja Baada ya Kujiuzulu

CCM Yamvua Uanachama Makamu wa Rais Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kumvua uanachama Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi.

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, leo Agosti 26, 2026, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba.

Dkt. Migiro amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kufanyika kwa vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM, vilivyokaa kujadili suala la maadili ya Dkt. Nchimbi ndani ya chama.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, vikao hivyo vilifikia uamuzi wa pamoja wa kumfuta uanachama Dkt. Nchimbi.

Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Dkt. Nchimbi, Agosti 25, 2026, kutangaza kujiuzulu nafasi yake ya Makamu wa Rais.

Akizungumza wakati wa kutangaza uamuzi huo, Dkt. Nchimbi alisema amejidhihirishia pasina shaka kuwa Rais Samia Suluhu Hassan anahitaji Makamu mwingine wa Rais.

Kujiuzulu kwake kumeongeza mabadiliko makubwa katika uongozi wa juu wa Serikali, huku hatua ya CCM ya kumvua uanachama ikifuata muda mfupi baada ya tangazo lake la kujiuzulu.

Leave a Comment