
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, imeendelea leo Agosti 27, 2026 katika Mahakama jijini Dar es Salaam, baada ya mwenendo wake kuahirishwa jana.
Katika mwenendo wa jana, upande wa Serikali uliendelea na hatua ya kumuuliza Lissu maswali ya dodoso baada ya kuwasilisha ushahidi wake wa kujitetea.
Mwendesha mashtaka Katuga alianza kwa kumuuliza Lissu kuhusu vielelezo alivyowasilisha mahakamani, ambapo Lissu alithibitisha kuwa vielelezo D1 hadi D15 ni vyake na kwamba ameridhika vitumike katika utetezi wake.

Katika sehemu nyingine ya mahojiano, Katuga alimuuliza Lissu kuhusu maana ya ulinzi wa mashahidi, ambapo Lissu alisema ni mashahidi wa kificho au wanaolindwa.
Lissu pia alihojiwa kuhusu madai yake kwamba baadhi ya watu waliokuwa ndani ya mahakama huenda walikuwa mashahidi waliolindwa. Alipoulizwa kama madai hayo yalikuwa ushahidi au hisia, Lissu alisisitiza kuwa ni ushahidi kwa sababu watu hao hawakujulikana na umma.

Lissu: Ni vyangu kwa sababu mimi ndiye niliyeomba viingizwe mahakamani.
Katuga: Je, nikisema kwamba uliomba vipokelewe mahakamani kama vielelezo vyako, umeridhika na yaliyomo ndani ya vielelezo hivyo?
Lissu: Ndiyo, nimeridhika.
Katuga: Umeridhika vitumike kama vielelezo vyako, na unaridhika na vielelezo ulivyovitoa?
Lissu: Nimeridhika vitumike katika utetezi wangu.
Katuga: Waheshimiwa Majaji, tunaomba vielelezo D1 hadi D15 …
Katuga: Naona tutakaa hapa siku mbili
Lissu: Unanitisha na siku mbili nimekaa ndani mwaka na miezi mitano
Katuga: Iambie mahakama ulinzi wa mashahidi maana yake nini
Lissu: Ni mashahidi wa kificho/ ni mashahidi wanaolindwa
Katuga: Iambie mahakama, Je, ulisema baadhi ya watu huenda tulikuwa nao humu ndani. Je, huu ni ushahidi au hisia tupu?
Lissu: Ndio ni shahidi wangu sababu hawajulikani hakuna anayewajua isipokua nyie
Katuga: Je ushahidi wa kwamba hawa ni mapolisi. Je, ni ushahidi au fununu tu?
Lissu: Ni ushahidi sababu hawajulikani na yeyote
Katuga: Sasa shahidi tunataka majibu sahihi ni kweli au sio kweli. Ushahidi wa kwamba baadhi ya mashahdi huenda tulikuwa nao humu ndani. JE, ni kweli, sio kweli, sio wa kuona wala kusikia?
Lissu: Sio Kweli
Katuga: Iambie mahakama kama ni kweli au sio kweli unatuhuma nyingie za kuchapisha uongo mtandaoni
Lissu: Ni kweli
Katuga: Iambie mahakama unakumbuka ulisomewa hoja za awali na ikaanza kusikilizwa
Lissu: Ndio nianakumbuka
Katuga: Unakumbuka uliposomewa hoja za wali ulisema majaji ni ma-CCM
Lissu: Sikumbuki
Katuga: Iambie mahakama hii katika hotuba yako pia ulitangaza kutokugombea kwa chama chako
Lissu: Sikumbuki, nakumbuka nilisema tutahamasisha ….
Katuga: Hapana, hukumbuki nimsekia ukijiita mwenyekiti wa Chadema. Iambie mahakama kama chama chako kilishiriki uchaguzi mwaka jana
Lissu: Hapana hakikushiriki
Katuga: Je, ni kweli kwamba uliposema mahakamani hakuendeki huna imani na mahakama
Lissu: Kwenye maswala haya ya uchaguzi sina imani na mahakama
Katuga: Kwenye zile njia ulizotuambia jana. Je, nitakuwa sahihi kwamba hukupanga kabisa kuiomba mahakama kutumia sheria
Lissu: Sikupanga kabisa
Katuga: Kwa hiyo ni sahihi kwamba swala la kupinga sheria kwa njia ya mahakama sio njia mbadala wala ya kidemokrasia
Lissu: Hapana
Katuga: Kwa hiyo kukinukisha ni njia ya kidemokrasia?
Lissu: Ndio ni njia ya kidemokrasia
Katuga: Kuhamasisha uasi ni njia ya kidemokrasia?
Lissu: Ndio ni njia ya kidemokrasia
Katuga: Uko Timamu mzee wangu
Lissu: Kimya
Katuga: Kama nilikusia ulitamka vifungu vya 55, 63, 52 kifungu cha 52 cha sheria ya habari. Ni kweli kwamba sheria ya habari iliundwa kwa ajili ya kuendesha tasnia ya habari?
Lissu: Ndio
Katuga: Kama nilikusikia vyema ulisema kuikosoa serikali sio kosa
Lissu: Nilisema kuipinga serikali sio kosa
Katuga: Kama una kanuni yako ya adhabu hapo kwa ridhaa ya mahakama hiki kifungu cha 55, yale maneno uliyotumbua, ‘ya kuzuia uchaguzi’ waambie majaji kuzuia uchaguzi ni kuipinga serikali au kuzuia uchaguzi?
Lissu: NI kuzuia uchaguzi
Katuga: Kuhamasisha uasi, kukinukisha nikupinga serikali au kupanga kuipindua serikali?
Lissu: Ni kuipinga serikali, sikuwa nazungumza habari ya serikali tulikuwa tunapanga kuzuia uchaguzi
Katuga: Unakumbuka umesema kwenye hotuba yako ulikuwa huzungumzii serikali
Lissu: Ndio sikuwa napinga serikali nilikua nazungumza habari za uchaguzi
Katuga: Kama nikikusikia vyema uliwaambia waheshimiwa hawa mashahidi wanaotoka jeshi la polisi, kasoro mmoja, wote wamejiandikia maelezo kitu ambacho ni kinyume cha sheria. Waambie majaji kama uliwatajia kifungu cha sheria na sheria yenyewe
Lissu: Sikuwaambia kifungu lakini kipo
Katuga: Unajua kwamba askari aliyemuandika shahidi maelezo na yeye ni shahidi kama huyo shahdi hata fika mahakani
Lissu: Sikumbuki
Katuga: Kama nilikusikia vyema uliiambia mahakama hii kwamba shahidi PW1 hakusema kama alivyogundua ni kosa la uhaini hakuwasiliana na ngazi za juu akiwemo DCI, kwamba ilipelelezwa vibaya
Lissu: nilisema ilipelelezwa vibaya
Katuga: Iambie mahakama kama sheria inaelekeza ukigundua kosa la uhaini lazima uwasiliane na hizo mamlaka zote, imabie mahakama kama ulitaja kifungu
Lissu: Hapana sikutaja kifungu
Katuga: Je unakumbuka ulisema kuna kutoelewana kati yako na Kingai (Kamishna wa Polisi Ramadhani Kingai ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) nchini Tanzania) pamoja na IGP Wambura (Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Camillius Wambura)
Lissu: Ni kweli nimekamatwa mara kadhaa bila kuzingatia taratibu
Katuga: Umekuwa mwanasheria muda mrefu na mwana siasa miaka 24. Je, ushawafunguliwa wawili hawa mashitaka?
Hapana: Sijawafungulia
Katuga: Kama nimekusikia vizuri uliambia mahakama hii kwamba wale mashahdi walioletwa ni mashahidi ambao walikuwa ni washitakiwa
Lissu: Nilisema walikiri kupanga uhalifu
Katuga: Je, kuna sheria inayozuia mtu aliyefanya uhalifu kuja kutoa ushahidi?
Lissu: Hapana
Katuga: Katika ushahidi wa mashahidi toka Jeshi la polisi walieleza walikamata wote
Lissu: Waliokamata waliweza kuwatambua
Katuga: Kwa ushahidi huo ina maana inawezekana kukawa na wengine
Lissu: Hawakutambuliwa au hawakukamatwa
Katuga: Nakukumbusha ile kauli yako si ndio uliambia mahakama mtu yeyote anaweza kutafsiri vyovyote vile na wale walisema wamehamasika kutokana na nini
Lissu: Maneno yangu
Katuga: Kwa hiyo nitakuwa sahihi nikisema walielewa hotuba yako na kufanyia kazi maneno yako kwa jinsi walivyoelewa
Lissu: Hapana siwezi sema sababu siwajui na siwezi kuwasemea
Katuga: Je, uliiambia mahakama hawa mashahidi ni waongo na hawastahili kuaminiwa na mahakama?
Lissu: Ndio, niliambia mahakama hawapaswi kuaminiwa wao na ushahidi wao