Xiaomi imezindua rasmi simu mpya za REDMI 17, zikiwa na kivutio kikubwa cha betri kubwa ya 7500mAh iliyowekwa kwenye mwili wenye skrini pana ya inchi 6.9. Hii ni hatua kubwa kwa watumiaji wanaochoshwa na kuchaji simu kila siku, kwani REDMI 17 inaahidi matumizi ya hadi siku tatu kwa chaji moja, kutegemeana na jinsi simu inavyotumika.
Betri Inayokupa Uhuru wa Siku Kadhaa
Ukubwa wa betri ya 7500mAh ndio kiini cha simu hii mpya. Kwa mujibu wa Xiaomi, betri hii inatosha kukuwezesha kutazama video kwa saa 28 mfululizo, au kusikiliza muziki kwa hadi saa 91 bila kuwa na wasiwasi wa betri kwisha katikati ya siku. Kwa mtumiaji wa kawaida anayetumia simu kwa mitandao ya kijamii, kupiga simu, na kutazama video mara kwa mara, hii inamaanisha unaweza kukaa hadi siku tatu bila kuhitaji chaja jambo linalofanya REDMI 17 kuwa chaguo bora kwa wasafiri, wafanyabiashara, na mtu yeyote asiyependa kubeba chaja kila mahali.
Turbo 45W: Chaji Haraka Inapohitajika
Ingawa betri kubwa mara nyingi huchukua muda mrefu kujaa, Xiaomi imetatua tatizo hilo kwa kuweka teknolojia ya turbo fast charging ya 45W. Hii inamaanisha, hata pale unapohitaji nishati ya haraka kabla ya kutoka nyumbani, REDMI 17 inaweza kujaa kwa haraka na kukuwezesha kuendelea na siku yako bila kusubiri kwa muda mrefu karibu na soketi.
Skrini Pana ya Inchi 6.9 kwa Matumizi Bora
- REDMI 17 inakuja na skrini kubwa ya inchi 6.9 yenye kiwango cha uonyeshaji cha 120Hz, jambo linalofanya michoro na video kuonekana laini na wazi zaidi. Skrini hii pia inalindwa na kioo imara cha Corning Gorilla Glass 7i, hivyo kuipa simu uimara zaidi dhidi ya mikwaruzo na michubuko ya kila siku. Aidha, simu ina kiwango cha ulinzi wa IP64 dhidi ya maji na vumbi, ikiongeza uhakika wa matumizi katika mazingira mbalimbali.

Kwa mchanganyiko wa betri kubwa ya 7500mAh, chaji ya haraka ya 45W, na skrini pana ya inchi 6.9, REDMI 17 inajipambanua kama moja ya simu bora za Xiaomi mwaka huu kwa watu wanaotanguliza muda mrefu wa matumizi ya betri bila kuathiri ubora wa uzoefu wa simu.