
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche, leo Septemba 10, 2026 amefika katika Ukumbi wa Mahakama kwa ajili ya kuendelea kutoa utetezi wake katika kesi ya uhaini namba 19605/2025, inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu.
Katika hatua hiyo ya kesi, Lissu alimtaka Heche kuieleza Mahakama kuhusu uzoefu wake na kile alichokiita “matatizo ya chaguzi za nchi.”

Akijibu, Heche amesema amewahi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi mara kadhaa, ikiwemo kuwa Diwani na Mbunge, pamoja na kushiriki katika kampeni mbalimbali za uchaguzi.
Heche pia ameeleza kuwa ameshiriki katika kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Arumeru, Geita, pamoja na kampeni za uchaguzi wa ubunge wa mwaka 2015 na 2020.
Ushahidi huo ni sehemu ya mwenendo wa kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu.
Lissu: Waeleze majaji, nilipokuja jimboni kwako mwaka 2020 nini kilitokea?
Heche: Waheshimiwa majaji, Lissu alikuwa mgombea urais wa CHADEMA mwaka 2020. Alifika jimboni kwetu, tukafanya mikutano maeneo kadhaa. Siku ya kwanza, kesho yake tulitarajia kufanya mikutano katika kata inayoitwa Matongo. Hili eneo linaitwa Kewanja. Polisi walituzuia kwa mabomu katika eneo ambalo mgombea alipaswa kusalimia wananchi. Kukatokea vurugu kubwa sana kati ya raia na polisi. Kulikuwa na maji ya washawasha, risasi na mabomu. Lakini vurugu zilipokuwa kubwa sana na polisi wakazidiwa, walituruhusu kufanya mkutano.
Heche: Lengo lilikuwa kutawanya watu wasije kutusikiliza. Kwa imani yao, tungekosa watu wa kutusikiliza. Bahati nzuri ilikuwa ni Tarime, Waheshimiwa Majaji, ambako si rahisi vitisho hivyo vikawakimbiza watu waliokuwa na hamu ya kumsikiliza mgombea urais.
Heche: Wakati mgombea wetu anafanyiwa hivi, hakuna mgombea wa CCM aliyewahi kufanyiwa hivyo. Si Magufuli wakati ule wala Samia sasa, ambaye mikutano yao imewahi kuharibiwa kwa mabomu, risasi na maji ya washawasha.
Lissu: Waeleze majaji, hili ni swali langu la mwisho kwa leo. Siku ya uchaguzi wa mwaka 2020 katika Jimbo la Rorya kulikuwa na nini?
Heche: Waheshimiwa majaji, siku ya uchaguzi mkuu katika Jimbo la Rorya, ambako alikuwa anagombea Ezekia Biogot Wenje ubunge kupitia CHADEMA, walivamiwa nyumbani kwao na polisi. Katika tukio hilo, ndugu Nyatenda Wenje aliuawa nyumbani kwao pamoja na kuwepo kwa Wenje.
Lissu: Huyu Nyatenda Wenje alikuwa nani?
Heche: Alikuwa ndugu yake wa Ezekia Wenje.
Lissu: Je, Ezekia Wenje kitu gani kilimtokea?
Heche: Katika tukio hilo, Bwana Ezekia Wenje alinusurika kuuawa. Alikimbilia Kenya na baadaye akaenda uhamishoni nchini Canada.
Lissu: Waeleze majaji, hatua zozote zilichukuliwa dhidi ya wauaji wa Nyatenda Wenje?
Heche: Waheshimiwa majaji, sina kumbukumbu yoyote juu ya hatua zilizochukuliwa dhidi yao.
Lissu: Waheshimiwa majaji, nimemaliza kwa leo.
Lissu: Naomba tuahirishe mpaka kesho ili tuendelee na examination-in-chief, Waheshimiwa Majaji.
Jaji: Upande wa mashitaka mnasemaje?
Nzengeli: Ni sawa, tuahirishe mpaka kesho.
Jaji: Shauri limeahirishwa. Uamuzi utatolewa kesho.
Lissu: Matukio mengine?
Heche: Wakati nagombea ubunge mwaka 2015, nilipokuwa naenda kufanya kampeni Kata ya Nyanungu, Tarime, tulishambuliwa na akauawa Bwana Bokhe Mwita Waitiei.
Lissu: Alishambuliwa na watu gani?
Heche: Alishambuliwa na wafuasi wa CCM. Walikamatwa na baadaye kuachiwa, kisha kesi ikaisha hivyo.
Lissu: Unamaanisha nini unaposema kesi ilifunguliwa?
Heche: Walikamatwa kwa sababu walifahamika, lakini baadaye waliachiwa huru.
Lissu: Nini kilitokea kwenye uchaguzi wa Busanda?
Heche: Aliuawa kiongozi Alphonce Mawazo, ambaye alikuwa mgombea wa Jimbo la Busanda. Hata kumzika ilibidi tuombe amri ya mahakama kwa sababu tulizuiwa kumuaga huku mwili wake ukiwa bado hospitalini.
Lissu: Alphonce Mawazo alikuwa na nafasi gani kwenye chama?
Heche: Alikuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita na mjumbe wa Baraza Kuu la chama.
Lissu: Kuna hatua zozote zilichukuliwa dhidi ya waliomuua Alphonce Mawazo?
Heche: Sikumbuki vizuri mwisho wa kesi hiyo, hivyo siwezi kueleza kwa uhakika.
Lissu: Waeleze majaji nini kilitokea jimboni kwako Tarime mwaka 2020.
Heche: Mwaka 2020, wakati nafunga kampeni Nyamongo, tulivamiwa kwa risasi. Watu wawili waliuawa na wengine kujeruhiwa. Waliouawa ni Chacha Isangora na Chacha Gabir.
Watu waliowashambulia wanafahamika. Maganda ya risasi yalikutwa eneo la tukio. Baadhi yao walikuwa viongozi wa CCM. Polisi walichukua maganda hayo, waliwashikilia kwa muda, lakini baadaye wakawaachia. Familia zimebaki na yatima na wajane kutokana na matukio yanayohusishwa na uchaguzi.
Lissu: Waeleze majaji kama kuna tukio lingine la wakati wa uchaguzi.
Heche: Kwenye uchaguzi hapana, lakini katika shughuli za siasa zipo nyingine. Polisi walimuua mdogo wangu.
Waheshimiwa majaji, mdogo wangu aliitwa Suguta Heche. Alikamatwa Sirari mwaka 2018, akafungwa pingu mikono nyuma na kuchomwa sindano akiwa katika hali hiyo.
Sirari ipo Tarime Vijijini. Baadaye kulikuwa na madai ya jaribio la kumtupa ili ionekane amepata ajali au ameshambuliwa na watu wasiojulikana. Walinzi wa eneo waliona kilichokuwa kinaendelea, hivyo akarudishwa kituo cha polisi.
RPC wa wakati huo alitoa taarifa kwa umma kwamba mdogo wangu ameuawa kikatili na polisi na kwamba hatua zingechukuliwa. Askari aliyekuwa anahusishwa na tukio hilo aliachiliwa na kuhamishwa kituo, na mpaka sasa ni mtumishi wa Jeshi la Polisi.
Ninaamini mdogo wangu aliuawa kutokana na msimamo wangu wa kisiasa na kupinga maovu ya nchi hii, na kwamba tukio hilo lilikuwa ujumbe kwamba wanaweza kufanya lolote bila hatua za kisheria kuchukuliwa.
Chanzo cha picha, Facebook/Heche
Lissu: Kiswahili cha No Reforms, No Election ni nini?
Heche: Bila mabadiliko hakuna uchaguzi.
Lissu: Ni mabadiliko gani yaliyoazimiwa na Kamati Kuu?
Heche: Kamati Kuu iliazimia mabadiliko ya kikatiba na kisheria ili kuondoa mamlaka makubwa ya Rais ya kuunda Tume ya Uchaguzi, wakati yeye mwenyewe ni mgombea. Ni kama simba anacheza na Yanga halafu Yanga ndiye anachagua refa.
Lissu: Una maana gani unapozungumzia tume?
Heche: Tume Huru ya Uchaguzi ambayo haitakuwa na upendeleo wala kuingiliwa na mgombea ambaye ana maslahi.
Lissu: Usinitangulie, ukinitangulia… anaonesha majaji wa serikali. (Kicheko mahakamani.)
Lissu: Shahidi, nataka uwaeleze majaji uzoefu wako na matatizo ya chaguzi za nchi hii.
Heche: Waheshimiwa majaji, mimi nimegombea mara kadhaa. Nimekuwa diwani na nimekuwa mbunge katika chaguzi za nchi hii. Nimeshiriki maeneo mbalimbali katika kampeni za chama.
Chaguzi zote hizi, waheshimiwa majaji, ziliambatana na maumivu makubwa; kutekwa, kuenguliwa kwa wagombea wetu, kuibiwa kwa fomu za viapo vya mawakala, ratiba zetu kuingiliwa na polisi, kupigwa kwa watu katika mikutano ya kampeni, wagombea wetu kunyimwa fomu za matokeo, kura za uongo kuingizwa kwa maboksi na mabegi na askari polisi ambao walitakiwa kusimamia uchaguzi. Wagombea wetu walienguliwa kwa kuambiwa hawajui kusoma na kuandika.
Naomba nitafafanua jambo moja baada ya jingine.
Nitaanza na mauaji.
Katika uchaguzi wa Arumeru, Katibu wetu wa USA River, Bwana Msafiri Bwambo, aliuawa kwa kuchinjwa kwa chainsaw. Watu waliosadikiwa kuwa wanachama wa CCM walihusishwa na tukio hilo, na mpaka leo hakuna mtu aliyekamatwa au kufungwa kwa mauaji hayo.
Lissu: Tukio lingine, shahidi.
Heche: Hapa Dar es Salaam, Kinondoni, aliuawa Mwenyekiti wa CHADEMA wa Ananasi, Dani Yona. Vilevile hakuna uchunguzi uliokamilika wala mtu aliyekamatwa, waheshimiwa majaji.
Mwanachama wetu Akwilina Akwilini, ambaye wakati huo Kamanda wa Polisi, Bwana Mambosasa, alithibitisha aliuawa kwa risasi ya polisi. Hakuna askari aliyekamatwa wala kushitakiwa.
Badala yake, nilishtakiwa mimi, John Mnyika, ambaye wakati huo alikuwa Katibu Mkuu; Freeman Mbowe ambaye alikuwa Mwenyekiti; Vincent Mashinji aliyekuwa Katibu Mkuu; Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini; Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini; Halima Mdee, Mbunge wa Kawe; Ester Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini; na Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.
Lissu: Waeleze majaji mlishtakiwa kwa kosa gani na kesi iliishia wapi?
Heche: Kwanza nieleze jambo moja. Wote hao walikuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya chama. Walishtakiwa kwa makosa mbalimbali, ikiwemo uchochezi na kushiriki kusanyiko lisilo na kibali.
Lissu: Kabla sijasahau, hiyo kadhia ilinikosaje mimi?
Heche: Waheshimiwa majaji, Mwenyekiti wetu wa sasa alikuwa ameshambuliwa vibaya kwa risasi na alikuwa akipatiwa matibabu nje ya nchi. Wakati huo alikuwa Makamu Mwenyekiti.
Lissu: Uamuzi wa hiyo kesi ulikuwaje?
Heche: Tulihukumiwa kifungo cha miezi sita au kulipa faini. Mimi nililipa faini ya shilingi milioni 40. Kwa ujumla ilikuwa karibu shilingi milioni 300.
Lissu: Ilikuwa katika mahakama gani?
Heche: Ilikuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, na ilisikilizwa na hakimu ambaye baadaye alipandishwa cheo na kuwa jaji.
Lissu: Baada ya kuhukumiwa, nini kilifuata?
Heche: Tulikata rufaa Mahakama Kuu, na baadaye hukumu ile ilitupiliwa mbali. Mahakama ikaamuru turejeshewe fedha zetu, lakini mpaka leo sijawahi kurejeshewa, licha ya amri hiyo.
Lissu: Ni jaji gani wa Mahakama Kuu aliyetoa amri hiyo?
Heche: Jaji Mgeta, waheshimiwa.
Lissu: Sasa shahidi, ulisema kulikuwa na mauaji ya Akwilina Akwilini. Hiyo habari iliishia wapi?
Heche: Kama zilivyo habari nyingine za mauaji.
Jaji: Tuambie iliishia wapi.
Heche: Iliishia hapo, na hakuna aliyeshitakiwa wala kufungwa kwa mauaji hayo.
Lissu: Kwa kuwa nimekuita utoe ushahidi katika kesi hii, waeleze majaji mimi ni mtu wa aina gani.
Heche: Namfahamu kama mzalendo, mwanademokrasia, mzalendo wa kweli, mpenda maendeleo ya nchi hii, muadilifu, mtu anayependa kushindanisha mawazo kwa hoja. Amekuwa mbunge, na kabla hata mimi sijaingia bungeni nilikuwa namfuatilia. Ni mtu jasiri asiyeogopa kusema ukweli. Kwa lugha yetu tunasema ni mpiganaji wa kweli.
Kwa sisi watu wa Tarime, nilimfahamu alipokuja kumtetea marehemu Chacha Wangwe na wananchi wa Nyamongo waliodai kunyang’anywa maeneo yao ya asili yaliyokuwa na madini ya dhahabu.
Lissu: Kwa nini umemtaja Mzee Augustino Sasi?
Heche: Mzee Augustino Sasi alikuwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Kewanja kupitia Chama Cha Mapinduzi na alifungwa kwa kile kilichoelezwa kuwa kesi za uonevu, ikiwemo kupokonywa mali zake.
Baada ya kutoka gerezani alijiunga na chama chetu na akachaguliwa kuwa diwani. Nilifanya naye kazi katika Baraza la Madiwani. Nilimkuta katika kipindi chake cha pili cha uongozi, kwa sababu mimi nilichaguliwa mwaka 2008.
Lissu: Waeleze majaji, kwa kumbukumbu zako, ni watu wangapi niliowatetea katika matatizo yao?
Heche: Ni kundi kubwa. Ninawakumbuka wachache kama kina Wangwe kwa sababu ilikuwa ni jambo kubwa sana Tarime wakati huo kutokana na uonevu uliodaiwa kufanyika.
Lissu: Sasa tuzungumze kuhusu kesi ambayo nimekuita utoe ushahidi wa utetezi. Waeleze majaji, kulikuwa na nini tarehe 3 Aprili mwaka jana?
Heche: Kulikuwa na kikao cha watia nia wa nafasi mbalimbali kupitia chama chetu. Tulikuwa nao katika kikao kilichofanyika Makao Makuu ya chama.
Lissu: Lengo la mkutano huo lilikuwa nini?
Heche: Lengo lilikuwa kuwaeleza kuhusu msimamo wa chama wa “No Reforms, No Election”.
Bila mabadiliko hakuna uchaguzi. Lengo lilikuwa kukutana nao na kuwaelimisha na kuwapa elimu kwa nini chama kimechukua msimamo huo kwenye maamuzi ya vikao vilivyokuwa vimetangulia mwezi wa 12, mwaka uliokuwa umeisha.”
Lissu: Hivyo vikao vilivyotangulia ni vikao gani na tarehe zake kama unakumbuka?
Heche: Nimekuwa mjumbe wa Kamati Kuu kwa muda mrefu, hivyo nilipata nafasi ya kushiriki vikao vya Kamati Kuu baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa, ambapo kulikuwa na malalamiko kwamba uchaguzi huo umeharibiwa kwa wagombea wa CHADEMA kuenguliwa nchi nzima. Watu waliuawa, ikiwemo Manyoni ambako mgombea wetu aliuawa, na pia Dar es Salaam hapa.