Hivi karibuni, video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii imemuonyesha mwanamke mmoja akiendesha baiskeli huku amembeba mtoto mgongoni, na nyuma akiwa amebeba tenga la matunda kwa ajili ya kufanya biashara.
Global TV imemtafuta mama huyo, aliyejitambulisha kwa jina la Bahati Rashidi Onyango, mkazi wa Mtaa wa Mtambani, Vingunguti jijini Dar es Salaam, na kuzungumza naye kuhusu maisha yake na namna anavyopambana kujikimu.

Bahati amesema aliamua kuanza biashara ya matunda baada ya awali kufanya biashara ya asali, lakini alikumbana na changamoto ya kutolipwa fedha zake.