×

Oman Yahairisha Mkutano Wa Kujadili Hatma Ya Mlango Wa Hormuz

Oman imetangaza kuahirishwa kwa mkutano uliokuwa umepangwa kujadili hatma ya Mlango wa Hormuz, njia muhimu inayotumika kusafirisha kiasi kikubwa cha mafuta na gesi duniani.

Wiki iliyopita, Iran ilitangaza kuwa Oman ingekuwa mwenyeji wa mkutano huo. Hata hivyo, hakuna nchi nyingine katika eneo hilo iliyothibitisha rasmi kushiriki, huku Bahrain ikitangaza wazi kuwa haitahudhuria.

Pamoja na kuahirishwa kwa mkutano huo, Oman imesema itaendelea kuhimiza mazungumzo yenye lengo la kuimarisha utulivu, usalama na ushirikiano wa kikanda.

Leave a Comment