
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, ameanza ziara nchini Hispania na kutembelea klabu ya FC Barcelona, ambako amekutana na Rais wa klabu hiyo, Joan Laporta.
Katika ziara hiyo, Makonda amefanya mazungumzo na viongozi wa Barcelona kuhusu fursa za ushirikiano katika maendeleo ya soka, kukuza vipaji, maendeleo ya kiufundi pamoja na maandalizi ya Tanzania kuelekea AFCON 2027.
Mazungumzo hayo pia yameangazia namna uzoefu na mfumo wa soka wa Barcelona unavyoweza kusaidia katika kuimarisha maendeleo ya mchezo wa soka nchini Tanzania.

Aidha, Makonda amemkabidhi Rais wa Barcelona, Joan Laporta, salamu za pole kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia msiba wa mume wake, Marehemu Hafidh Ameir Hassan, pamoja na kumkabidhi barua ya rambirambi kwa ajili ya kumfikishia Rais Samia.

Makonda pia anatarajiwa kushuhudia mchezo wa FC Barcelona dhidi ya Racing Santander, utakaochezwa Jumatano, Septemba 16, 2026, katika uwanja wa Spotify Camp Nou.
Kwa kifupi: Ziara hiyo inalenga zaidi katika kujenga ushirikiano wa kimichezo kati ya Tanzania na FC Barcelona, hususan katika maendeleo ya vipaji na soka la Tanzania kuelekea AFCON 2027.
Stori na Tereza Muga | GPL -TUDACO