×

Aunty Ezekiel na Kusah Wawasha Instagram kwa Picha za Mahaba

STAA wa Bongo Movie, Aunty Ezekiel, amemwandikia ujumbe wa kimahaba mume wake, mwanamuziki, Salmin Ismail Hoza ‘Kusah’, katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa leo Septemba 18, 2026.

Aunty Ezekiel, kupitia chapisho lake lenye picha za pamoja wakiwa gym, amemueleza Kusah kuwa hana maneno mengi ya kuandika, badala yake amemtaka asikilize wimbo aliouambatanisha na ujumbe huo.

“Hata sina cha kuandika, sikiliza tuu hii nyimbo. Then tuanzie hapo! 😊🥰 Ntaendelea kesho 😘 Picha la…. 😅 HAPPY BDAY HONEY ❤️,” ameandika Aunty Ezekiel.

Ujumbe huo ulivuta hisia za Kusah, ambaye naye alijibu kwenye sehemu ya maoni kwa maneno ya upendo huku akimuita Aunty Ezekiel “mama wa wanangu.”

“NAKUPENDA MAMA WA WANANGU ‘TUPO SANA’ 😂✊,” ameandika Kusah.

Baada ya ujumbe huo, mashabiki pamoja na baadhi ya mastaa waliingia kwenye maoni wakionyesha kufurahishwa na namna wawili hao wanavyooneshana upendo.

Baadhi yao waliandika jumbe za kuwatakia heri, huku wengine wakitania kuhusu picha zao za kimahaba na uhusiano wao.

Maoni hayo yalijumuisha ujumbe kama “Nawapenda sana,” “I love this,” pamoja na “Nikiwa mkubwa nataka kuwa kama wewe na shemeji.”

Wengine walitumia nafasi hiyo kumtakia Kusah heri ya kuzaliwa huku wakieleza kufurahishwa na ukaribu unaoonekana kati yake na Aunty Ezekiel.

Chapisho hilo limeendelea kuzua gumzo miongoni mwa mashabiki wao, hasa kutokana na ujumbe wa kimahaba wa Aunty Ezekiel na jibu la Kusah linaloonesha ukaribu wao.

Leave a Comment