
Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amefanya mazungumzo na viongozi wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA).
Kikao hicho kimefanyika leo, Ijumaa, Septemba 18, 2026, katika Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni, jijini Dar es Salaam.
Katika kikao hicho, Waziri Mkuu amekutana na wawakilishi wa wamiliki wa mabasi nchini kwa ajili ya mazungumzo kuhusu masuala yanayohusu sekta ya usafirishaji kwa njia ya mabasi.
