×

G Nako Na Live Band Kutikisa Jukwaa, Wasanii Wengine Kukiwasha

Nguli wa muziki G Nako (Warawara) anatarajiwa kulipua jukwaa katika kilele cha Gambe Fest 2026 tarehe 03/10/2026, akitumbuiza mubashara na Live Band pamoja na wasanii wengine wakubwa.

Kilele hicho kinatarajiwa kuwa na performance ya hatari kutoka kwa G Nako & Live Band, sambamba na wasanii waalikwa, Guest DJs, Guest Artists, Karaoke Battle, Live Band Experience, Fashion Bonanza, Sip & Shop, Acrobatic & Fire Shows na michezo kibao ya kushirikisha mashabiki.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Masoko wa Mi Casa Lounge, Denis Binamungu, amesema Gambe Fest 2026 linatua rasmi kuanzia tarehe 20/09/2026 hadi 03/10/2026, likiahidi wiki mbili za msisimko wa hali ya juu na burudani isiyo na kikomo katika Mi Casa Lounge, Barabara ya Mandela, Ubungo.

Amesema burudani hizo zitaenda sambamba na Live BBQ, ambapo mashabiki watapata nyama choma na msosi wa mkaa papo hapo muda wote wa tamasha.

Kwa mujibu wa Binamungu, tiketi tayari zimeanza kuuzwa kupitia @otapptz na Mi Casa Lounge, Mandela Road, Ubungo, huku mashabiki wakitarajiwa kupata mchanganyiko wa muziki, burudani, michezo na burudani shirikishi kwa siku zote za Gambe Fest 2026.

Leave a Comment