×

Matumizi Bora ya Nishati na Safari Mpya ya Jetour Nchini Tanzania…

Kuongezeka kwa gharama za nishati na changamoto za upatikanaji wa mafuta duniani kumeendelea kuongeza umuhimu wa matumizi ya magari yenye teknolojia inayoweza kupunguza utegemezi wa mafuta.

Kwa Tanzania, Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imekuwa ikisisitiza matumizi bora na yenye ufanisi ya nishati, pamoja na hatua za kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ya mafuta.

Katika mwelekeo huo, JETOUR Tanzania imezindua JETOUR Club na kutambulisha magari mawili mapya ya teknolojia ya plug-in hybrid, JETOUR G700 na JETOUR F700, yanayowawezesha watumiaji kutumia umeme na mafuta kulingana na mahitaji ya safari zao.

Hatua hiyo inalenga kuongeza chaguo kwa Watanzania wanaohitaji magari yenye uwezo wa kusafiri katika mazingira mbalimbali huku yakitoa fursa ya kutumia umeme katika safari fupi na mafuta katika safari ndefu, tofauti na magari yanayotegemea mafuta pekee.
Uzinduzi huo umefanyika chini ya kaulimbiu ya “Africa Expedition 2025”, ukiwa sehemu ya mpango wa JETOUR Tanzania, kwa kushirikiana na Africarriers Group, wa kuimarisha uwepo wa chapa hiyo katika soko la Tanzania na wakati huo huo kuunganisha teknolojia ya magari ya kizazi kipya na uzoefu mpana wa umiliki.
Mkurugenzi Mtendaji wa JETOUR Tanzania, Zain Pirbhai, amesema kampuni hiyo inalenga kuwapa wateja magari yanayokidhi mahitaji ya matumizi ya kila siku, safari za masafa marefu pamoja na shughuli za nje, huku teknolojia ya plug-in hybrid ikitoa unyumbufu katika matumizi ya nishati.

Kwa upande wake, Mohamed Ladha, Mkuu wa Kitengo cha Masoko, amesema JETOUR F700 ni pickup ya plug-in hybrid yenye injini ya turbo ya lita 2.0, mota mbili za umeme na mfumo wa Two-Speed Dedicated Hybrid Transmission.

Amesema gari hilo lina uwezo wa kuzalisha hadi kW 665, sawa na horsepower 892, torque ya Nm 1,135, kuvuka maji yenye kina cha hadi milimita 900 na kuvuta mzigo wa hadi tani 3.5. Aidha, linaweza kutoa umeme wa nje wa hadi kW 20.

Amesema teknolojia hiyo inawezesha matumizi ya umeme kwa safari fupi na injini ya petroli kwa safari ndefu.

 

Leave a Comment