
Msanii maarufu wa sanaa ya uigizaji nchini, Irene Uwoya, ameendelea kuteka mitandao ya kijamii baada ya kushirikisha picha zake mpya zilizowavutia mashabiki, huku sehemu ya maoni ikijaa sifa na jumbe za kumpongeza.
Uwoya, ambaye ni miongoni mwa mastaa wanaofuatiliwa kwa karibu kwenye mitandao ya kijamii, amekuwa akiwapa mashabiki wake burudani kupitia picha na mitindo mbalimbali anayoshirikisha kwenye ukurasa wake.

Katika moja ya machapisho yake ya hivi karibuni, mwigizaji huyo aliambatanisha picha hiyo na maneno mafupi “UWOYA … one piece 👑”, ujumbe ulioonekana kuongeza hamasa kwa mashabiki wake kuacha maoni mbalimbali.
Muda mfupi baada ya picha hiyo kuwekwa, mashabiki walimiminika kwenye sehemu ya maoni huku wengi wakimsifia kwa muonekano wake.

Baadhi ya mashabiki waliandika, “SEE BEAUTY ,” “Umependeza sana kipenzi ,” na “Queen dizaina,” huku wengine wakitumia emoji za moto, mapenzi na makofi kuonyesha kuvutiwa na picha hizo.
Shabiki mmoja kutoka Kenya pia alitoa ujumbe akisema, “Love You from Kenya,” jambo linaloonyesha kuwa Uwoya anaendelea kupata ufuasi kutoka kwa mashabiki nje ya Tanzania pia.

Katika chapisho jingine, mashabiki waliendelea kumiminika na maoni ya kumsifia, huku baadhi wakisema “We mdada mkari bwana,” “Aaaah we ninja kabisa,” “Ze shuuuuzi” na “Kiatu mama .”

Wengine walimuita “Mrembo,” “Queen” na kutumia emoji za moyo na moto, huku idadi ya likes kwenye baadhi ya maoni ikionyesha mwitikio mkubwa kutoka kwa wafuasi wake.
Kwa mwitikio huo, ni wazi kuwa kila Uwoya anaposhirikisha picha zake mpya, mashabiki wake huwa tayari kumpokea kwa jumbe za sifa na pongezi.

Irene Uwoya ni miongoni mwa majina yanayojulikana katika tasnia ya burudani nchini, na mbali na kazi zake za uigizaji, amekuwa akitumia mitandao ya kijamii kuwasiliana na mashabiki na kushirikisha sehemu mbalimbali za maisha na mitindo yake.