×

Rais Samia Ateua Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Halmashauri

Dodoma, Septemba 29, 2026 — Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali wa Serikali, akiwemo Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya pamoja na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi na uhamisho huo unahusu viongozi katika maeneo mbalimbali nchini na umeanza mara moja.

 WAKUU WA WILAYA WATEULIWA

Katika ukurasa wa kwanza, Rais Samia amewateua Wakuu wa Wilaya 22.

Walioteuliwa ni:

  1. Nicodemus Tambo Mwikozi – Mkuu wa Wilaya ya Arusha
  2. Maiko Richard Kachoma – Mkuu wa Wilaya ya Chato
  3. Edwin Mathew – Mkuu wa Wilaya ya Tanga
  4. Zaytun Seif Swai – Mkuu wa Wilaya ya Korogwe
  5. Atupele Frank Mwakibete – Mkuu wa Wilaya ya Kilolo
  6. Mtella Allam Mwampamba – Mkuu wa Wilaya ya Uvinza
  7. Musa Ramadhani Sima – Mkuu wa Wilaya ya Newala
  8. Sozi George Ngate – Mkuu wa Wilaya ya Chunya
  9. Mwana Rajabu Kambangwa – Mkuu wa Wilaya ya Mbulu
  10. SACP Selemani Enock Nyakulingaa – Mkuu wa Wilaya ya Kibondo
  11. Luteni Kanali Robert Augustino Kakomangile – Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro
  12. Luteni Kanali Fortunatus Beda Kipeta – Mkuu wa Wilaya ya Kibiti
  13. Luteni Kanali Joseph Athanas Murimi – Mkuu wa Wilaya ya Kasulu
  14. Festo Kiswaga – Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe
  15. Neema Lugangira – Mkuu wa Wilaya ya Arumeru
  16. Vita Rashid Kawawa – Mkuu wa Wilaya ya Hanang’
  17. Richard Atufigwege Kas esera – Mkuu wa Wilaya ya Mvomero
  18. Dkt. Francis Daudi Mlacha – Mkuu wa Wilaya ya Kahama
  19. Mwita Petro Marwa – Mkuu wa Wilaya ya Masasi
  20. Stanlaus Shing’oma Mabula – Mkuu wa Wilaya ya Rorya
  21. Christopher Andendekisye Kitwika – Mkuu wa Wilaya ya Uyui
  22. Mwanaidi Adadi Rajabu – Mkuu wa Wilaya ya Pangani.

Uhamisho wa Wakuu wa Wilaya

Taarifa hiyo pia imetaja uhamisho wa Wakuu wa Wilaya mbalimbali, akiwemo Grace Henry Kingalame aliyehamishwa kutoka Nyang’wale kwenda Meatu, Fauzia Hamidu Ngatumbura kutoka Meatu kwenda Kilindi, Hashim Shaibu Mgandilwa kutoka Kilindi kwenda Babati na Almishi Issa Hazali kutoka Hanang’ kwenda Kongwa.

Viongozi wengine waliohamishwa ni Mayeka Simon Mayeka kutoka Kongwa kwenda Urambo, Dkt. Khamis Athumani Mkanachi kutoka Urambo kwenda Nyang’wale, Kanali Isack Anton Mwakisu kutoka Kasulu kwenda Mis enyi, Michael John Semindu kutoka Mbulu kwenda Sikonge, Mwinyi Ahmed Mwinyi kutoka Arumeru kwenda Mkuranga, Peter Ambrose Lijualikali kutoka Nkasi kwenda Kalambo, Nickson Simon John kutoka Kibaha kwenda Songwe, Fadhil Emmanuel Nkur u kutoka Songwe kwenda Kibaha, Halima Habib Okash kutoka Chemba kwenda Mafia na Rukia Ally Zuberi kutoka Mwanga kwenda Hai.

UHAMISHO WA WAKUU WA WILAYA NA MAKATIBU TAWALA

Uhamisho wa Wakuu wa Wilaya uliendelea ambapo Hassan Omary Bomboko amehamishwa kutoka Hai kwenda Mwanga, Dkt. Khalfan Boniface Haule kutoka Rorya kwenda Bunda, Maulid Hassan Dotto kutoka Mvomero kwenda Malinyi na Amina Nassoro Makilagi kutoka Nyamagana kwenda Magu.

Aidha, Jubilate Win Lauwo amehamishwa kutoka Magu kwenda Nyamagana, Aziza Ally Mangosongo kutoka Mafia kwenda Chemba, Wilman Kapenjana Ndile kutoka Songea kwenda Ileje, Ng’olo Ng’wanidu hu Malenya kutoka Namtumbo kwenda Songea, Frank John Nkinda kutoka Kahama kwenda Mkalama, Hamad Rajab Mbega kutoka Mbozi kwenda Namtumbo, Farida Salum Mgomi kutoka Ileje kwenda Mbozi na Mohamed Mussa Mtulyakw aku kutoka Uyui kwenda Nkasi.

Makatibu Tawala wa Wilaya

Rais Samia pia amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Wilaya 12.

Walioteuliwa ni pamoja na:

  • Ali Said Ali – Temeke
  • Imani Lunogelo Fute – Kongwa
  • Mwanaid Ramadhani Nondo – Songea
  • Jane Daniel Mallongo – Nyang’wale
  • Leah Mbeke – Hanang’
  • Shabani Ferdinand Manyama – Bunda
  • Mjata Daffa Abdallah – Bahi
  • Florida Julius Lulandala – Moshi
  • Shaaban Mursadi Mteng eti – Mbozi
  • Juma Nyasa Juma – Rufiji
  • Jafari Abdallah Kikoti – Korogwe
  • Alexander Alfonse Mhando – Singida.

UHAMISHO WA MAKATIBU TAWALA NA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI

Kwa upande wa uhamisho wa Makatibu Tawala wa Wilaya, Mwanamvua Bakari Muyombo amehamishwa kutoka Bahi kwenda Simanjiro, Upendo Marango kutoka Kibondo kwenda Masasi, Fatima Said Kubenea kutoka Masasi kwenda Kibondo, huku Athumani Saidi Lik eyekeye akihamishwa kutoka Hanang’ kwenda Newala.

Wakurugenzi Watendaji Wateuliwa

Rais Samia amewateua pia Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri mbalimbali.

Miongoni mwa walioteuliwa ni:

  • Elikana Daud Zabron – Pangani
  • Agape Peter Fue – Sengerema
  • Samson Abas Sanga – Madaba
  • Warda Abeid Maulid – Manispaa ya Kibaha
  • Charles Ambokile Mwaitega – Mtama
  • Winfrid Erneus Tamba – Longido
  • Dinah Edward Msuya – Manyoni
  • Anna Lazaro Urio – Mkinga
  • Rashid Juma Muhaya – Kibondo.

UTEUZI NA UHAMISHO WA WAKURUGENZI

Uteuzi wa Wakurugenzi uliendelea ambapo Felix Joseph Tinkasimile ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Niceforus Martin Mgaya – Kishapu, Idrisa Musa Naumanga – Kyerwa, Dadi Horace Kolimba – Manispaa ya Mtwara Mikindani, William Mathew Makufwe – Njombe, Shaban Juma Mchomvu – Mufindi, Ramadhani Ali Kimara – Kibiti na Naima Bakari Chondo – Muheza.

Uhamisho wa Wakurugenzi

Kwa upande wa uhamisho, Fatima Hussein Laay amehamishwa kutoka Bukoba kwenda Kwimba, Anderson David Msumba kutoka Mtama kwenda Bukoba, James Michael John kutoka Kyerwa kwenda Lushoto, Ikupa Mwasyoge kutoka Lushoto kwenda Rombo na Philimon Mwita Magesa kutoka Namtumbo kwenda Jiji la Tanga.

Aidha, Juma Hamsini Seph amehamishwa kutoka Jiji la Tanga kwenda Manispaa ya Kigoma, Kisena Magena Mabuba kutoka Manispaa ya Kigoma kwenda Kilosa.

Uhamisho uliendelea ambapo Beatrice Claver Mwinuka amehamishwa kutoka Kilosa kwenda Namtumbo, Happiness Joachim Msanga kutoka Karagwe kwenda Kisarawe, Upendo Eric Mangali kutoka Manispaa ya Sumbawanga kwenda Manispaa ya Moshi na Jamal Idrisa Abdul kutoka Ml imba kwenda Manispaa ya Kigamboni.

Vilevile, Diocles Mugishagwe Rutema amehamishwa kutoka Kibondo kwenda Wilaya ya Itilima, Binuru Mussa Shekidele kutoka Sengerema kwenda Siha, Sunday Ndori Deogratius kutoka Ludewa kwenda Nyang’wale na Husna Toni Chambo kutoka Nyang’wale kwenda Masalala.

Wengine ni Duncan Golden Thebas kutoka Newala kwenda Mwanga, Mashaka Said Mfaume kutoka Mufindi kwenda Karagwe, Majid Hemed Mwanga kutoka Mlele kwenda Manispaa ya Mpanda, Hellen Mwambeta kutoka Siha kwenda Manispaa ya Shinyanga, Rehema Said Bwasi kutoka Mji wa Mbulu kwenda Mlele na Bosco Addo Ndunguru kutoka Manispaa ya Musoma kwenda Misungwi.

ORODHA YA MWISHO YA UHAMISHO

Uhamisho ulihitimishwa kwa viongozi wengine akiwemo:

  • Hassan Nyange – kutoka Manispaa ya Mtwara Mikindani kwenda Mji wa Mbulu
  • Khalid Khalif – kutoka Nyasa kwenda Ludewa
  • Dkt. Peter Maiga Nyanja – kutoka Wanging’ombe kwenda Mji wa Makambako
  • Anastazia Tutuba Ruhamwya – kutoka Manyoni kwenda Manispaa ya Musoma
  • K uruthum Amour Sadick – kutoka Mji wa Njombe kwenda Manispaa ya Sumbawanga
  • Sajidu Idrisa Mohamed – kutoka Madaba kwenda Nyasa
  • Abdallah Nandonde – kutoka Mbozi kwenda Newala
  • Emmanuel Johnson Matinyi – kutoka Kishapu kwenda Wanging’ombe
  • Hanan Mohamed Bafagih – kutoka Wilaya ya Kibiti kwenda Manispaa ya Ubungo
  • Christopher Aloyce Sanga – kutoka Njombe kwenda Malinyi
  • Kenneth Kenneth Haule – kutoka Mji wa Makambako kwenda Mtama.

Taarifa hiyo, iliyotolewa Dodoma Septemba 29, 2026, imesainiwa na Bakari S. Machumu, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, na inaeleza kuwa uteuzi na uhamisho huo unaanza mara moja.

Leave a Comment