×

Ajira Mpya: LUHETI Yatangaza Nafasi za Daktari, Muuguzi na Wengine

Njombe. Taasisi ya Mafunzo ya Afya Lug arawa (LUHETI), iliyoanzishwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Njombe, imetangaza nafasi tano za kazi kwa Watanzania wenye sifa, katika kada mbalimbali za afya, TEHAMA na maktaba.

Taasisi hiyo, ambayo ipo katika Wilaya ya Ludewa, Mkoa wa Njombe, ilianzishwa mwaka 1998 na inafanya kazi kwa mujibu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), kwa namba REG/HAS/036.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, nafasi zilizotangazwa ni Daktari (MD), Afisa Muuguzi Daraja II (Nursing Officer), Afisa Teknolojia Maabara Daraja II (Medical Laboratory Scientist), Mkutubi (Librarian) na Afisa TEHAMA (ICT), ambapo kila nafasi inahitajika mtu mmoja.

Waombaji wa nafasi ya Daktari wanatakiwa kuwa na Shahada ya Udaktari na kuwa wamehudhuria mafunzo ya Teaching Methodology. Kwa Afisa Muuguzi Daraja II, mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Uuguzi na mafunzo ya Teaching Methodology, huku Afisa Teknolojia Maabara akitakiwa kuwa na Shahada ya Sayansi ya Maabara Tiba pamoja na mafunzo hayo.

Kwa upande wa nafasi ya Mkutubi, mwombaji anatakiwa kuwa na Diploma au zaidi katika fani ya Maktaba. Nafasi ya Afisa TEHAMA inahitaji mwombaji mwenye angalau Diploma katika TEHAMA, Sayansi ya Kompyuta, Multimedia, Masoko ya Kidijitali au fani inayohusiana, pamoja na uzoefu wa angalau miaka miwili na vielelezo vya kazi alizowahi kufanya (portfolio).

Waombaji wametakiwa kuwasilisha barua ya maombi, CV pamoja na nakala za vyeti vya elimu na taaluma kwa Mkuu wa Taasisi, Taasisi ya Mafunzo ya Afya Lug arawa (LUHETI), S.L.P. 389, Njombe, au kutuma maombi kupitia barua pepe principall [email protected]. Mwisho wa kupokea maombi ni Oktoba 16, 2026.

Leave a Comment