×

Jihan Arejea Tanzania kwa Mara ya Kwanza Akiwa Miss Grand International 2026 – Video

Mshindi wa taji la Miss Grand International 2026, Jihan, amerejea nchini Tanzania kwa mara ya kwanza tangu kutwaa taji hilo la kimataifa, akiongozana na Rais wa Miss Grand International, Mr. Nawat

Mshindi wa taji la Miss Grand International 2026, Jihan, leo Oktoba 17, 2026 amerejea nchini Tanzania kwa mara ya kwanza tangu kutwaa taji hilo la kimataifa, huku akiongozana na Rais wa Miss Grand International, Mr. Nawat, aliyefika kushiriki naye furaha ya kurejea nyumbani na kusherehekea ushindi wake wa kihistoria.

Kurejea kwa Jihan nchini Tanzania kumeashiria mwanzo wa ukurasa mpya katika safari yake ya urembo na uwakilishi wa kimataifa. Ingawa hafla rasmi ya kumkaribisha nyumbani bado inatarajiwa kufanyika, tayari kurejea kwake kumeleta hisia za furaha, fahari na upendo kwa malkia huyo.

Mashabiki na Watanzania wanatarajia kumpokea Jihan kwa shangwe na nderemo katika hafla rasmi ya Homecoming, itakayokuwa fursa ya kusherehekea mafanikio yake na ushindi unaoiweka Tanzania katika mwanga wa kimataifa.

Karibu nyumbani, Queen Jihan! Tanzania inajivunia wewe!

 

Leave a Comment