
Katika ulimwengu wa michezo, ushindi hauishii uwanjani pekee, bali pia katika maisha ya kila siku ya jamii. Hii ndiyo falsafa inayoendelea kuoneshwa na Meridianbet kupitia juhudi zake za kurudisha kwa jamii, safari hii ikigusa maisha ya Mama Lishe na Baba Lishe wa Kata ya Mbezi Juu, jijini Dar es Salaam. Kampuni hiyo ya ubashiri imekabidhi vifaa vya usafi wa mazingira kwa wafanyabiashara hao, ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) unaolenga kuboresha mazingira na ustawi wa wananchi.
Zoezi hilo limefanyika kwa kushirikiana na Diwani wa Kata ya Mbezi Juu, Anna Lukindo, likiwa na lengo la kuhamasisha utunzaji wa mazingira na kuweka maeneo ya biashara katika hali ya usafi na usalama. Kama ilivyo katika mchezo wa soka ambapo kila mchezaji ana jukumu muhimu katika kuleta ushindi wa timu, kila mwananchi ana nafasi ya kuhakikisha mazingira yanayomzunguka yanakuwa safi. Kupitia msaada huo, Meridianbet inaonesha kuwa maendeleo ya jamii yanahitaji ushirikiano, mshikamano na hatua za vitendo zinazogusa maisha ya watu moja kwa moja.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya MERIDIANBET au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Vifaa hivyo vinatarajiwa kuwasaidia Mama Lishe na Baba Lishe kukusanya na kutunza taka katika maeneo maalumu badala ya kuzitupa ovyo. Hatua hii ni muhimu kwa sababu mazingira safi yanachangia kulinda afya ya wananchi, kuvutia wateja na kuboresha shughuli za biashara za kila siku. Kwa wafanyabiashara wanaohudumia watu kwa chakula, usafi ni sehemu muhimu ya huduma bora.
Akizungumzia msaada huo, Nancy Ingram kutoka Meridianbet amesisitiza umuhimu wa kushirikiana na viongozi wa maeneo husika pamoja na makundi mbalimbali ya kijamii ili kutatua changamoto zinazowakabili wananchi. Ushirikiano na Diwani Anna Lukindo unaonesha namna sekta binafsi na serikali za mitaa zinavyoweza kuunganisha nguvu katika kuleta mabadiliko chanya.
Meridianbet imetoa wito kwa Mama Lishe, Baba Lishe na wananchi kwa ujumla kutumia vifaa hivyo ipasavyo, kutunza maeneo yao na kuendeleza utamaduni wa kutupa taka katika sehemu zilizotengwa. Kupitia mpango wake wa CSR, kampuni hiyo inaendelea kuthibitisha kuwa dhamira yake si kushiriki katika burudani ya michezo na ubashiri pekee, bali pia kuwa sehemu ya suluhisho la changamoto zinazokabili jamii.