×

Rais Samia Amfariji IGP Wambura Baada ya Kifo cha Baba Yake (Picha +Video)

Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akimfariji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Camillus Wambura, nyumbani kwake Masaki Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Oktoba, 2026, kufuatia kufiwa na Baba yake mzazi Deusdedit Mwita Wambura aliyefariki tarehe 24 Oktoba, 2026 Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemtembelea na kumfariji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura, nyumbani kwake Masaki, jijini Dar es Salaam, leo Jumanne, Oktoba 27, 2026, kufuatia kifo cha baba yake mzazi, Deusdedit Wambura.

Deusdedit Wambura amefariki dunia Oktoba 24, 2026, jijini Dar es Salaam. Katika ziara hiyo, Rais Samia ametoa pole kwa IGP Wambura na familia yake, akiwafariji katika kipindi hiki kigumu cha majonzi kufuatia kuondokewa na mpendwa wao.

Ziara hiyo ya rambirambi imeonesha mshikamano na faraja kwa familia ya Mkuu wa Jeshi la Polisi katika kipindi cha maombolezo. Familia, ndugu na jamaa wanaendelea kuomboleza kifo cha Deusdedit Wambura, huku wakipokea pole kutoka kwa watu mbalimbali.

P

 

Leave a Comment