
Rais wa Jamhuri ya Angola, João Manuel Gonçalves Lourenço, amewasili jijini Dodoma, Oktoba 30, 2026 akitokea jijini Dar es Salaam kwa kutumia reli ya kisasa ya SGR.
Mhe. Joao Manuel Gonclves Lourenco amefika jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya ziara yake nchini kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kihostoria na kukuza ushirikiano wa kiuchumi wa pande mbili katika sekta mbalimbali.

Safari hiyo ya kihistoria kwa Rais Lourenço kutumia Reli ya SGR, imeonesha umuhimu wa matumizi ya miundombinu ya kisasa ya usafiri wa reli nchini Tanzania, huku viongozi hao wakiendelea na ratiba ya ziara hiyo jijini Dodoma ikiwemo uzinduzi rasmi wa Mji wa Serikali uliopo Mtumba jijini humo.
