×

Oura Awaokoa Simba, Aipa Ushindi Dhidi ya Namungo Uwanja wa Uhuru

DAR ES SALAAM: Mshambuliaji Anicet Oura amekuwa shujaa wa Simba SC baada ya kuifungia timu hiyo bao la tatu na kuipa uongozi wa mabao 3-2 dhidi ya Namungo FC katika mchezo unaopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Oura alianza kuandika jina lake kwenye mchezo huo kwa kufunga bao la kwanza dakika ya tatu, akiipa Simba SC mwanzo mzuri wa mchezo.

Hata hivyo, Namungo FC walirejea kwa nguvu kupitia Lulendi aliyefunga mabao mawili dakika ya 35 na 43, na kuifanya timu hiyo ya kusini kwenda mbele kwa mabao 2-1.

Simba SC iliendelea kupambana kutafuta matokeo, kabla ya De Reuck kusawazisha kwa mkwaju wa penalti dakika ya 79 na kurejesha matumaini kwa mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi.

Dakika ya 88, Oura alikamilisha kazi yake kwa kufunga bao la tatu la Simba SC, na kuifanya timu hiyo kuongoza kwa mabao 3-2 katika dakika za mwisho za mchezo.

Ushindi huo unaendelea kuonesha ushindani mkubwa wa mchezo huo, huku Oura akiibuka kuwa mchezaji muhimu kwa Simba SC kutokana na mabao yake mawili.

Leave a Comment