
Dodoma, 21 Oktoba 2026 – Uongozi wa Airtel Tanzania umeipongeza timu ya Airtel Kanda ya Kati kwa utendaji kazi wa mfano na kufikia malengo chini ya kauli mbiu ya “StepUp 2026/27”. Mafanikio haya yanadhihirisha wazi nia thabiti ya timu hiyo katika kuleta mageuzi chanya na kuboresha namna ya utoaji huduma kwa wateja.
Hafla ya Simba la Masimba ilifanyika rasmi jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Charles Kamoto. Dhamira ya hafla hiyo ni kutambua juhudi za pamoja za wafanyakazi, ikiwemo kujituma, nidhamu na ushirikiano ambao umechangia mafanikio ya kanda hiyo.
Katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Charles Kamoto, aliipongeza timu ya Airtel kwa juhudi na mchango wa kila mmoja katika kuleta mabadiliko chanya na kukuza biashara ya Airtel Tanzania.
“Tunapaswa kusherehekea… kusherehekea juhudi ambazo kila mmoja wetu anazifanya katika kuendeleza biashara ya Airtel Tanzania. Santosh Kumar ameongoza katika kuhamasisha ushindani na kuanzisha mpango huu wa kuvunja rekodi za malengo kupitia Simba la Masimba, na vijana wanapambana,” alisema Kamoto.
Kamoto alimpongeza Mkurugenzi wa Mauzo na Usambazaji wa Airtel Tanzania, Santosh Kumar kwa kuongoza juhudi za kuanzisha mpango wa Simba la Masimba na kuhamasisha ari ya ushindani chanya miongoni mwa timu.
Mbali na kutambua mafanikio, Simba la Masimba StepUp 2026/27 unawahimiza wafanyakazi kuongeza juhudi katika kuwahudumia wateja, kuimarisha uwepo wa Airtel na kutimiza ahadi ya kampuni ya kutoa mawasiliano ya uhakika na huduma bora. Kwa kujenga utamaduni wa uwajibikaji na kuimarisha ushirikiano. Simba la Masimba inaunga mkono azma ya Airtel Tanzania ya kukidhi mahitaji ya wateja na kuhudumia makundi mbalimbali ya wateja kama vile watu binafsi, familia, taasisi, wajasiriamali na biashara Kila Kona.
Kwa upande wake, Kumar alisema “Pigeni hatua na mkaache alama!” Kiongozi huyo aliwahimiza vijana wanaoanza safari yao ya kikazi kuwa na shauku ya maendeleo, kuonesha uwezo wao mkubwa, na kuacha alama chanya isiyosahaulika kwa Watanzania wote kupitia mchango wao kwa jamii Kila Kona.
Kupitia Simba la Masimba, Airtel Tanzania inaendelea kuimarisha utamaduni wa utendaji unaozingatia matokeo, ambapo mafanikio ya wafanyakazi yanachangia kufikia lengo kubwa zaidi la kuboresha huduma kwa wateja, kuimarisha mawasiliano na kuongeza thamani kwa wateja.
Wakati timu za Airtel zikiendelea kupiga hatua kote nchini, kampuni ya Airtel inaendelea kuhakikisha kuwa mafanikio yake yanatafsiriwa katika huduma bora na mahusiano mazuri zaidi na wateja wake, Kila Kona.