
Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza mabadiliko katika uongozi wa Ikulu ya White House kwa kumwondoa Susie Wiles katika nafasi ya Mkuu wa Watumishi wa Ikulu (Chief of Staff), na kumteua mshauri wake wa karibu, Stephen Miller, kuchukua nafasi hiyo kuanzia Jumatatu, Novemba 9, 2026.
Trump ametangaza uamuzi huo kupitia mtandao wake wa Truth Social, akisema Miller, ambaye kwa sasa ni Naibu Mkuu wa Watumishi wa Ikulu, ni miongoni mwa washauri anaowaamini zaidi. Pia amempongeza Wiles kwa kazi yake na kueleza kuwa atahamia katika shughuli za kisiasa za Trump (Trump Political Operation).

Kwa mujibu wa taarifa za CBS News na Reuters, mabadiliko hayo yanakuja siku chache baada ya Chama cha Republican kupata matokeo mabaya katika uchaguzi wa katikati ya muhula (Midterm Elections), ambapo Democrats walipata ushindi muhimu na kurejesha udhibiti wa Bunge la Marekani. Taarifa hizo zinaeleza kuwa kuondoka kwa Wiles kunahusishwa na matokeo hayo, ingawa Ikulu haijatoa sababu rasmi ya mabadiliko hayo.
Stephen Miller, mwenye umri wa miaka 41, amekuwa mshauri wa Trump tangu kampeni za uchaguzi wa mwaka 2016 na anajulikana kuwa mmoja wa watu waliohusika kwa kiasi kikubwa kuandaa sera kali za serikali kuhusu uhamiaji na kuwafukuza wahamiaji wasio na vibali. Uteuzi wake unatarajiwa kuimarisha ushawishi wake katika maamuzi ya utawala wa Trump.
Kwa upande wake, Wiles, ambaye alikuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo katika historia ya Marekani, amesema kuhudumu katika Ikulu chini ya Trump kumekuwa heshima kubwa kwake. Alikuwa msimamizi muhimu wa kampeni za Trump za mwaka 2024 na amekuwa Mkuu wa Watumishi wa Ikulu tangu Trump aliporejea madarakani Januari 2025.