
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewaapisha viongozi wanne kuwa wajumbe wa Kamati ya Usaili wa Wajumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, Novemba 9, 2026.
Viongozi walioapishwa ni Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Ndugu Dunford George Mpelumbe, na Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo, Ndugu Omar Ali Omar Bhai, ambao wameapishwa kuwa wajumbe wa Kamati hiyo.

Wengine ni Jaji Mkuu wa Tanzania, George Masaju, aliyeapishwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, pamoja na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Khamis Ramadhan Abdalla, aliyeapishwa kuwa Makamu Mwenyekiti.
Uundwaji wa Kamati hiyo unatokana na Kifungu cha 9 (1) cha Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Na. 2 ya mwaka 2024, huku Kifungu cha 9 (2) kikielekeza wajumbe wa Kamati hiyo kula kiapo mbele ya Rais kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yao.

