×

TFF Yatangaza Majina ya Wanaonia Tuzo za Msimu 2025/26, Kufanyika Arusha Desemba 12, 2026

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza majina ya wachezaji, makocha, waamuzi na wadau mbalimbali walioingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo za msimu wa 2025/26, huku hafla ya utoaji wa tuzo hizo ikitarajiwa kufanyika Desemba 12, 2026, jijini Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF Novemba 11, 2026, tuzo hizo zimegawanywa katika makundi mbalimbali yanayohusisha Ligi Kuu ya NBC, Kombe la Shirikisho la CRDB, Ligi Kuu ya Wanawake, ligi nyingine pamoja na tuzo za utawala na heshima. Jumla ya tuzo zitakazotolewa ni 38, huku watakaowania wakiwa 61.

Leave a Comment