
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Novemba 12, 2026, ameongoza mjadala kuhusu Nishati Safi ya Kupikia Barani Afrika katika Mkutano wa Ngazi ya Juu uliofanyika pembezoni mwa Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31), nchini Uturuki.
Mkutano huo umefanyika katika Kituo cha Mikutano cha ANFAŞ Antalya Expo Center, ambapo Rais Samia ameshiriki kuongoza majadiliano yanayohusu suala la upatikanaji na matumizi ya nishati safi ya kupikia barani Afrika, eneo ambalo linahitaji ushirikiano wa wadau mbalimbali katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

Mjadala huo una umuhimu mkubwa kwa nchi za Afrika kutokana na changamoto zinazoendelea kuikabili bara hilo katika upatikanaji wa nishati safi ya kupikia, ambapo matumizi ya nishati zisizo safi bado ni suala linalohitaji hatua za pamoja.
Matumizi ya nishati safi ya kupikia yanatajwa kuwa miongoni mwa hatua muhimu za kulinda afya za wananchi, kupunguza uchafuzi wa mazingira na kupunguza utegemezi wa nishati zinazochangia uharibifu wa misitu na ongezeko la hewa ukaa.

Ushiriki wa Rais Samia katika mjadala huo ni sehemu ya shughuli zake katika Mkutano wa COP31, unaowakutanisha viongozi wa mataifa mbalimbali, taasisi za kimataifa na wadau wa mazingira kujadili hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.



