×

Trump Atoa Kauli ya Kushtua Kuhusu Vita vya Iran, Asitisha Mazungumzo

Rais wa Marekani, Donald Trump.

WASHINGTON, Marekani – Rais wa Marekani, Donald Trump, amuelekeza Makamu wa Rais JD Vance kuelekeza nguvu zake zote katika kushughulikia madai ya udanganyifu, uhalifu na rushwa katika miji na majimbo yanayoongozwa na chama cha Democratic, hatua inayomuweka pembeni katika juhudi za kidiplomasia za kutafuta suluhu ya vita dhidi ya Iran.

Trump ametoa maelekezo hayo Alhamisi, Novemba 12, 2026, siku moja baada ya gazeti la Wall Street Journal kuripoti kuwa Vance alikuwa akifikiria kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na kiongozi mwandamizi wa usalama wa Iran.

Kupitia mtandao wake wa Truth Social, Trump alisema Marekani haihitaji tena makubaliano na Iran kwa kuwa kipindi cha kufanya hivyo kimepita.

Makamu wa Rais wa Marekani, JD Vance

“Hatuhitaji makubaliano na Iran. Siku hizo zimepita muda mrefu. Tuna fedha zao, mamia ya mabilioni ya dola, na tuna Mlango-Bahari wao wa Hormuz,” aliandika Trump.

Kauli hiyo imekuja wakati Marekani ikiendelea kuweka vikwazo vya kiuchumi na kuzuia shughuli za bandari za Iran, huku jeshi lake likijaribu kuhakikisha usafirishaji wa kimataifa unafanyika kwa usalama kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz.

Jeshi la Iran lilisema Alhamisi kuwa meli nne za mafuta zilishambuliwa kwa milipuko baada ya kupuuza maonyo yaliyotolewa na vikosi vyake, hali inayoongeza wasiwasi kuhusu usalama wa usafirishaji wa nishati katika eneo hilo.

Vance alikuwa na nafasi muhimu katika juhudi za kutafuta suluhu ya vita hivyo, ambapo aliongoza mazungumzo na maafisa wa Iran nchini Pakistan mwezi Aprili, yaliyofanikisha kupatikana kwa hati ya makubaliano ya maelewano mwezi Juni iliyosimamisha mapigano kwa muda kabla ya kuvunjika ndani ya wiki chache.

Mwezi uliopita, vyombo vya habari vya serikali ya Iran viliripoti kuwa Tehran ilikuwa imepokea barua kutoka kwa Vance iliyolenga kufungua tena mazungumzo na Washington. Hata hivyo, Trump alisema hakuwa amemwagiza makamu wake kuanzisha mawasiliano hayo.

Wakati huohuo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, alisema Jumanne baada ya mazungumzo na washirika wa Marekani mjini Paris kuwa madai ya Iran kuhusu masharti ya makubaliano, yakiwemo kutaka fidia ya uharibifu wa vita, hayakubaliki kwa upande wa Washington.

Mabadiliko ya msimamo wa Trump pia yanafuatia kushindwa kwa chama chake cha Republican katika uchaguzi wa katikati ya muhula, ambapo Democrats walipata ushindi mkubwa.

Vance, ambaye kwa muda mrefu ameonesha mashaka kuhusu vita vilivyoanzishwa na Marekani na Israel dhidi ya Iran mwezi Februari, alitaja gharama za vita hivyo kuwa miongoni mwa sababu zilizochangia kushindwa kwa Republican katika uchaguzi huo.

Pia alisema ushauri wake wa awali wa kusitisha vita ulikuwa ushauri sahihi.

Hata hivyo, Trump aliendelea kutetea hatua za kijeshi dhidi ya Iran, akisema zilikuwa muhimu kuzuia nchi hiyo kupata silaha za nyuklia.

Katika maelekezo yake mapya, Trump amemtaka Vance kuongoza juhudi za kuchunguza madai ya udanganyifu katika miji na majimbo yanayoongozwa na Democrats, akidai hatua hiyo inaweza kusaidia kusawazisha bajeti ya Marekani.

“Bajeti yetu inaweza kusawazishwa haraka kwa kurekebisha shughuli hizi kubwa za uhalifu. Rushwa iko ndani ya damu ya uongozi wa Democrats,” aliandika Trump.

Hatua hiyo inakuja wakati Vance akitajwa kuwa miongoni mwa wanasiasa wanaoweza kuwania urais kupitia chama cha Republican katika uchaguzi wa mwaka 2028, huku vita vya Iran vikiendelea kuwa suala muhimu katika siasa za ndani za Marekani.

Leave a Comment