
Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera imetangaza nafasi tatu (3) za kazi za kujitolea kwa Watanzania wenye sifa za kuajiriwa kama Dereva Daraja la II.Tangazo hilo limetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba tarehe 13 Novemba 2026, kwa kuzingatia Mwongozo wa Kujitolea katika Utumishi wa Umma wa mwaka 2025.
1. Nafasi zinazotangazwa
-
-
Cheo: Dereva Daraja la II
-
-
-
Idadi ya nafasi: 3
-
-
-
Aina ya ajira: Kujitolea
-
-
-
Mwajiri: Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
-
-
-
Mahali pa kazi: Bukoba, Kagera
-
2. Sifa za mwombaji
Mwombaji anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:
-
-
Awe na cheti cha Kidato cha Nne (Form IV).
-
-
-
Awe na leseni ya udereva daraja E au C.
-
-
-
Awe na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali.
-
-
-
Awe na vyeti vya mafunzo vilivyomwezesha kupata madaraja husika ya leseni.
-
-
-
Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya udereva (Basic Driving Course) kutoka VETA au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
-
3. Majukumu ya kazi
Dereva atakayepata nafasi atakuwa na majukumu yafuatayo:
-
-
Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kuhakikisha usalama wake.
-
-
-
Kuwasafirisha watumishi katika safari za kikazi.
-
-
-
Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
-
-
-
Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
-
-
-
Kujaza na kutunza taarifa za safari katika daftari la safari.
-
-
-
Kufanya usafi wa gari.
-
4. Masharti ya jumla ya waombaji
Mwombaji anatakiwa kuzingatia masharti yafuatayo:
-
-
Awe raia wa Tanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18 hadi 35.
-
-
-
Asiwe amewahi kuajiriwa katika taasisi yoyote ya umma.
-
-
-
Aandae wasifu binafsi (Detailed CV) wenye anwani, namba za simu zinazopatikana na majina ya wadhamini (Referees) watatu.
-
-
-
Aambatishe nakala za vyeti vya taaluma zilizothibitishwa na Mwanasheria au Wakili wa Serikali.
-
5. Nyaraka zinazotakiwa kuambatanishwa
Mwombaji anatakiwa kuwasilisha nakala za nyaraka zifuatazo:
-
-
Kitambulisho cha Taifa au namba ya NIDA.
-
-
-
Picha mbili za pasipoti za rangi.
-
-
-
Cheti cha kuzaliwa.
-
-
-
Cheti cha Kidato cha Nne.
-
-
-
Cheti cha Kidato cha Sita kwa waliofikia kiwango hicho.
-
-
-
Vyeti vya mafunzo mbalimbali yanayohusiana na nafasi husika.
-
-
-
Nakala ya leseni ya udereva.
-
-
-
Barua ya maombi ya kazi iliyosainiwa.
-
-
-
Wasifu binafsi (CV).
-
Muhimu: Testimonial, Provisional Results, Statement of Results na hati za matokeo ya Kidato cha Nne na Sita (Results Slips) hazitakubaliwa.
Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wanatakiwa kuhakikisha vyeti vyao vimethibitishwa na mamlaka husika, zikiwemo TCU, NECTA na NACTE.
Pia, mwombaji atakayebainika kuwasilisha taarifa au vyeti vya kughushi atachukuliwa hatua za kisheria.
6. Jinsi ya kutuma maombi
Barua za maombi zinapaswa kuelekezwa kwa:
MKURUGENZI MTENDAJI (W),
Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba,
S.L.P 491,
Bukoba, Kagera.
7. Mwisho wa kutuma maombi 25 Novemba 2026
Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi
Waombaji wanashauriwa kuwasilisha maombi yao kabla ya tarehe ya mwisho.
Kwa maelezo zaidi:
-
-
Simu: 028 2220287
-
-
-
Nukushi: 028 2221839
-
-
-
Barua pepe: [email protected]
-
-
-
Tovuti: www.bukobadc.go.tz
-
Ushauri kwa waombaji: Hakikisha nyaraka zote zimekamilika, vyeti vimethibitishwa na barua yako ya maombi imesainiwa kabla ya kuwasilisha.