×

Ujerumani Yaichapa Uholanzi Mabao 5-0 Katika Uefa Nations League

Timu ya Taifa ya Ujerumani imeendeleza ubabe wake baada ya kuichapa Uholanzi mabao 5-0 katika mchezo wa UEFA Nations League uliopigwa kwenye dimba la Olympiastadion jijini Berlin.

Katika mchezo huo, Ujerumani ilihitaji dakika 41 kupata bao la kwanza kupitia Scherhant, kabla ya kipindi cha pili kuwa kigumu zaidi kwa Uholanzi kufuatia mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa wenyeji.

Dakika ya 60, Florian Wirtz aliiongezea Ujerumani bao la pili, huku Schlotterbeck akifunga bao la tatu dakika ya 65 na kufanya Uholanzi kuzidi kupoteza mwelekeo wa mchezo.

Wirtz alirejea tena kwenye orodha ya wafungaji dakika ya 71 kwa kufunga bao lake la pili katika mchezo huo, kabla ya Gruda kuhitimisha karamu ya mabao dakika ya 77 na kuifanya Ujerumani kupata ushindi mnono wa mabao 5-0.

Matokeo hayo yanaifanya Ujerumani kupata ushindi wa kujivunia dhidi ya wapinzani wao wa jadi, Uholanzi, huku Florian Wirtz akiibuka miongoni mwa nyota walioacha alama kubwa katika mchezo huo kwa kufunga mabao mawili.

Leave a Comment