
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Arusha uliopo Kisongo, mkoani Arusha, Novemba 19, 2026, baada ya kuhitimisha ziara yake ya kitaifa nchini Uganda.
Baada ya kuwasili, Rais Samia alipokelewa na kusalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Amos Makalla.
Ziara hiyo ya kitaifa nchini Uganda ilikuwa sehemu ya shughuli za kidiplomasia za kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Uganda.
