×

Samia na Museveni Wazindua Kiwanda cha Kuunganisha Magari Nchini Uganda (Picha +Video)

Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akivuta kitambaa pamoja na Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda, kama ishara ya uzinduzi Kiwanda cha Kuunganisha Magari cha Double Q Automotive Assembly Plant kilichopo Mpigi nchini Uganda, tarehe 19 Novemba, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa pamoja na Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, wamezindua rasmi Kiwanda cha Kuunganisha Magari cha Double Q Automotive Assembly Plant kilichopo Mpigi nchini Uganda.

Uzinduzi huo umefanyika Novemba 19, 2026, ambapo viongozi hao walivuta kitambaa kufungua rasmi kiwanda hicho, ikiwa ni ishara ya kuanza kwa shughuli zake.

Uzinduzi huo unaashiria hatua muhimu katika kukuza sekta ya viwanda, uwekezaji na ushirikiano wa kiuchumi katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akikata utepe pamoja na Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda, kama ishara ya uzinduzi Kiwanda cha Kuunganisha Magari cha Double Q Automotive Assembly Plant kilichopo Mpigi nchini Uganda, tarehe 19 Novemba, 2026.
Rais Samia na Yoweri Kaguta Museveni wakitembelea Kiwanda cha Double Q Automotive Assembly Plant kilichopo Mpigi nchini Uganda.
Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akizungumza na Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda, baada ya kuwasili katika eneo la Kiwanda cha Kuunganisha Magari cha Double Q Automotive Assembly Plant kilichopo Mpigi nchini Uganda, tarehe 19 Novemba, 2026.

Leave a Comment