MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, ametembelea banda la Benki ya NMB katika Mkutano wa Madini na Uwekezaji Tanzania 2026, ambapo ameelezwa kuhusu fursa za kifedha zinazotolewa na benki hiyo kwa wachimbaji na wadau wengine wa sekta ya madini.
Katika ziara hiyo iliyofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam, Makamu wa Rais alipokelewa na Mkuu wa Idara ya Miamala wa Benki ya NMB, Linda Teggisa, aliyemweleza kuhusu masuluhisho ya kifedha yanayolenga wachimbaji wadogo, wa kati na wakubwa pamoja na biashara zinazohudumia sekta hiyo.
Huduma zilizoangaziwa ni pamoja na mikopo kwa wachimbaji, huduma za miamala na malipo pamoja na masuluhisho ya kibenki ya kidijitali, yanayolenga kurahisisha shughuli za kifedha na kusaidia wadau wa sekta hiyo kuendesha na kupanua biashara zao.
Ushiriki wa Benki ya NMB katika mkutano huo unaonesha dhamira ya benki hiyo ya kuendelea kusaidia upatikanaji wa mitaji na kuchochea uwekezaji katika sekta ya madini, ambayo ina nafasi muhimu katika uzalishaji, ajira na ukuaji wa uchumi wa Tanzania.

.jpeg)

.jpeg)